MANISPAA YA MOROGORO YATOA SHUKRANI KWA RAIS SAMIA KUPATIWA GARI LA TASAF
MANISPAA ya Morogoro, imetoa shukrani za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hasssan, kutona na kukabidhiwa gari mpya itakayotumiwa na Ofisi ya TASAF.
Pongezi hizo, zimetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, julai 10/2022 katika hafla fupi ya kukadhi gari hilo kwa Maratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro.
Machela,amesema kuwa agari hilo limekabidhiwa kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
“Tumepokea gari hili likiwa limekamilika kila kitu, utunzaji ni muhimu sana, lakini sikatai kutumika katika shughuli nyengine, yanaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za halmashauri pale kunapokuwa na shughuli nyingine za kiujumla lakini kipaumbele ni shughuli za TASAF, isitokee shughuli za TASAF zikashindwa kufanyika kwa kukosekana usafiri ni wajibu wa Afisa usafirishaji na dereva wa gari hili kuwa na mawasiliano ya kina na Ofisi ya TASAF kama kuna shughuli nyengine zinahitaji kufanyika kwa kutumia gari hilo”Amesema Machela.
Naye Maratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana, amesema gari hilo watalitunza na litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
ikumbukwe kuwa Rais Samia alifanya hafla hiyo ya kukabidhi magari ya TASAF katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022 ambapo jumla ya magari 241 yamekabidhiwa kwa Halamshauri ikiwa ni njia ya kuimarisha shughuli za utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Post a Comment