Header Ads

KUJIUNGA NA BIMA YA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF ILIYOBORESHWA).

 


Kujiunga na Bima ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa)

KUJIUNGA NA HUDUMA YA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF ILIYOBORESHWA)

Hatua Muhimu za Kuzingatia ili Kujiunga Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa):

  • Mkuu wa kaya fika na familia yako katika sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya uandikishaji wa wanachama.
  • Lipia gharama ya kujiunga na CHF iliyoboreshwa, hakikisha unapatiwa stakabadhi ya malipo ya mchango wa CHF.
  • Fuata maelekezo mengine utakayopewa na Afisa Uandikishaji.

Hakikisha kila mwanakaya amepatiwa kitambulisho cha uanachama.

Kumbuka:

  • Kitambulisho chako kitaanza kutumika mara baada ya kujiandikisha katika mfuko huo. 
  • Kumbuka kwenda na kitambulisho chako pindi unapokwenda kwenye kituo cha kutolea huduma (Zahanati, Kituo cha Afya au Hospitali ya Wilaya/Mkoa).
  •  Kumbuka kuhuisha/kufufua uanachama wako miezi miwili kabla ya kuisha muda wa uanachama.
  • Uanachama huhuishwa kila mwaka (mara moja kwa mwaka) kwa kulipia gharama ya uanachama.

Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) ni Nini?

Ni mpango muhimu wa hiari ulioanzishwa kwa Sheria Na. 1 ya mwaka 2001 (Sura ya 409 ya Sheria za Tanzania Toleo la 2002) wa kaya, kikundi au familia au mtu binafsi kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.

Wanachama wanapopata huduma bora ya afya kwa kipindi cha mwaka mzima.

Kaya/Familia ni Nini kwa Mujibu wa CHF Iliyoboreshwa?

Baba, mama n watoto/wategemezi ambao jumla yao ni watu sita (6).

Kundi la watu sita (6) katika taasisi kama vile shule (wanafunzi), Ushirika (wanaushirika), ama Vikundi vya ujasiria mali (SACCOS, VICOBA, n.k).

Mtu binafsi.

Faida za Mfuko wa Afya ya Jamii:

Mwanachama atanufaika na huduma zote za afya ya msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ya wilaya, kama vile;

Huduma ya wagonjwa wa kutwa na kulazwa kwa mujibu wa mwongozo wa Wizara ya Afya.

 Afya ya mama na mtoto.

Vipimo vya maabara.

Huduma ya upasuaji mdogo.

Mwanachama anapata huduma bora za afya kwa gharama nafuu.

Mwanachama anapata huduma bora ya afya kwa kipindi cha mwaka mzima.

Serikali inachangia kiasi sawa na kile kilichochangwa na wanachama tele kwa tele) katika wilaya husika ili kuboresha huduma za afya.

Ushiriki wa Mwanachama Katika Kuboresha Utoaji wa Huduma za Afya:

Mwanachama atashiriki katika kuboresha huduma za Afya kupitia mwakilishi wa jamii katika bodi ya Afya ya Wilaya na kamati za uendeshaji na usimamizi wa Kituo cha Afya na Zahanati.

Mwanachama atawasilisha mawazo/kero zake kwenye serikali ya kijiji, na kupelekwa kwenye kamati ya CHF ya kata na hatimaye kwenye bodi ya CHF ya wilaya ambayo itayajadili na kuyatolea maamuzi.

Pia, mwanachama ataweza kutoa maoni yake kuhusu maboresho ya CHF na huduma za Afya kupitia mkutano wa mwaka wa kijiji wa wanachama wa CHF.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisi ya Kijiji/Mtaa iliyokaribu nawe.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.