Header Ads

IJUE JUMUIYA YA WAZAZI CCM.



 

UTANGULIZI

Umoja wa Wazazi wa CCM uliundwa mwaka 1955 ikiwa ni mwaka mmoja tuu tangu kuundwa kwa Chama cha TANU mwaka 1954. Umoja huu uliundwa ukiwa na misingi mikuu miwili, Elimu pamoja na Malezi. Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Wazazi.

MAJUKUMU YA JUMUIYA YA WAZAZI.

• Kuhamasisha wazazi na Watanzania wa Rika zote juu ya umuhimu wa Elimu pamoja na kuanzisha na kusimamia shule za Jumuiya.
• Kusimamia Maadili na Malezi bora kwa Vijana na Jamii kwa ujumla ili kujenga Taifa lenye maadili na linalosimamia misingi ya utamaduni wa Kitanzania.
• Kusimamia Rasilimali pamoja na shughuli za kiuchumi zilizopo, na kubuni miradi mipya, kwa manufaa ya Jumuiya na Taifa kwa Ujumla.

DIRA

Kuwa Jumuiya ya mfano kwa kuhakikisha inatekeleza majukumu ya Jumuiya kwa ufanisi na Uadilifu na kuhakikisha misingi na maadili ya Chama inasimamiwa kikamilifu kwa ustawi wa Jumuiya na Chama cha CCM kwa ujumla.

DHIMA

Kuhakikisha kuwa malengo ya Jumuiya na Chama cha Mapinduzi katika kuboresha maisha ya Watanzania yanafanikiwa kwa kusimamia kazi za Jumuiya, Sera na Ilani za CCM kwa ufanisi, Uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.

MALENGO

Kuhakikisha kuwa Wazazi kama nguzo ya jamii wanashiriki katika ustawi wa Chama na Taifa kwa kusimamia Elimu, Malezi na Maadili kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinakua imara na madhubuti siku zote.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.