Header Ads

 




MADIWANI WAFURAHISHWA NA KAZI ZA WAJASILIAMALI.


Madiwani wa Manispaa ya Morogoro wametembelea maonyesho ya nane nane leo Agosti 8,2022 kwa ajili ya kujifunza tekinolojia mbalimbali mpya za Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kutembelea Banda na vipando vya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere.


Ikiwa ndio siku ya mwisho ya maonyesho ya nane nane ya Kanda ya Mashariki, Waheshimiwa Madiwani wakizunguka katika mabanda na vipando vya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamevutiwa na kazi nzuri za wajasiliamali hasa kwenye ubunifu wa kufuga samaki na kulima mboga za majani kwa kutumia maji ya kufugia samaki. Ubunifu huo unaweza kuotesha mboga bila kutumia mchanga na mbolea yeyote kwasababu maji hayo ya kufugia samaki yanakuwa na virutubisho vya kutosha vinavyowezesha kuotesha mmea bila changamoto yeyote.


Pia Waheshimiwa Madiwani wamefurahishwa sana na Lishe Tiba, wajasiliamali wengine wamejikita kutafuta tiba za magonjwa mbalimbali kupitia mimea au mchanganyo wa nafaka mbalimbali, jambo ambalo ni la kuwahakikishia wa Tanzania kuwa na Afya Bora na kufuta utapia mlo.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ametoa shukrani za dhati kwa Wajasiliamali wote kwa kushiriki nasi katika maonyesho hayo na kuwaomba kujipanga kimalifu katika maonyesho ya jayo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.