MANISPAA YA MOROGORO KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MASOKO YA NDANI
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro ipo mbioni kuboresha miundombinu ya masoko ya ndani ili yawe rafiki kwa wafanyabiashara.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana Oktoba 13/2022 katika ziara ya kamati hiyo ya kukagua miradi ya Masoko.
Kalungwana, amesema lengo la Manispaa ni kuboresha maeneo ya masoko pamoja na wafanyabiashara wake ikiwa ni mpango mkakati wa kuboresha masoko yote ya ndani ili kuiwezesha miradi hiyo kuwaingizia kipato cha mtu mmoja mmoja na Manispaa kwa ujumla.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Hamis Kilongo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihonda, amemshukuru Mkurugenzi pamoja na Baraza la Madiwani kwa kuiwezesha Kata yake kuwa na Soko licha ya kuwepo kwa changamoto.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Jeremia Lubeleje, amesema tayari Manispaa ishatenga fedha muda na wakati wowote masoko yataanza kuboreshwa ili wafanyabiashara wafanye biashara katika mazingira rafiki.
Lubeleje ,amesema kuwa kuboreshwa masoko ya ndani yatachangia ongezeko la pato la Halmashauri kama ilivyo kwa miradi mingine ikubwa ikiwamo wa Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro , Mawezi ,Nanenane pamoja na Masoko mengine ya ndani.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa leo na Kamati hiyo ni pamoja na Kutembelea eneo la mnada katika Soko la Azimio Kihonda, Soko la Mwanzomgumu Mwembesongo na kutembelea eno la mnada Soko la Kilakala.
Post a Comment