Header Ads

RAS MOROGORO AWATAKA MADIWANI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO





KATIBU Tawala Mkoa wa Morogoro, Dr. Mussa Ali Mussa,amewataka madiwani kusimamia miradi ya maendeleo katika kata zao  ili miradi hiyo kujengwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 27/2022 katika Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro uliofanyika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.

Akizungumza katika Mkutano huo, Dr. Mussa,amesema fedha nyingi zimekuwa zikilietwa na Serikali hivyo Madiwani wanatakiwa  kusimamia miradi iliyoko katika maeneo yao ili kuepuka maelekezo mengine watakapochelewesha miradi yanayoweza kusababisha utekelezaji ukawa kwa kiwango cha chini.

’Tushirikiane tuweze kumaliza miradi hii kwa wakati maana ukiwa wa mwisho unaanza kupokea maelekezo mengi sana na kwakuwa timu zote macho yatakuwa kwako unaanza kufanya kwa haraka kwa kulipua kitu ambacho sio sawa’’ Amesema Dr. Mussa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amesema Manispaa imepokea fedha nyingi za ujenzi wa madarasa shilingi Bilioni 1.6 hivyo kama ujenzi huo hautasimamiwa kikamilifu na kuchelewa itakuwa ni kitu kibaya ambacho watakuwa wamemuangusha Rais Samia.

Kwa upande wa Menyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma,  amewataka  wazazi kuchangia chakula kwaajili ya wanafunzi shuleni ili halmashauri hiyo iweze kuwa na maendeleo zaidi kielimu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.