MKUTANO WA WANANCHI MTAA WA MTAMBANI.
Leo Feb 07,2021.
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala ameshiriki katika Mkutano wa Wananchi katika Mtaa wa Mtambani.
Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani Kata ya Vingunguti chini ya Mwenyekiti wake ndugu Omary Kabatele umewasilisha taarifa ya kazi kwa Wananchi wa Mtambani. Mkutano huwo ambao Mgeni Rasmi alikuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti Mhe. Omary Kumbilamoto.
Mhe. Kumbilamoto ametoa shukrani kwa Wananchi wa Mtaa wa Mtambani kwa kukichagua cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Katika Mkutano huwo ilijitokeza changamoto ya maji ambapo Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala amemuagiza Mtendaji wa Kata kuitisha kikao siku ya jumatano katika Ofisi yake, lengo la kikao hicho ni kuwataka jumuia ya watumia maji Mtambani watoke kwenye utiaji wa saini katika Akaunti ya bank kwani mradi huwo wa maji kwa sasa umehama kutoka Halmashauri kwenda Dawasa na Akaunti hiyo inakuwa chini ya Mtendaji Kata.
Kikao hicho kitawakutanisha watu wa Dawasa, jumuia ya watumia maji Mtambani pamoja na watia saini kwenye Akaunti ya watumia maji Mtambani.
Aidha Mhe. Kumbilamoto ameeleza Dawasa wanashindwa kutoa fedha kwaajili ya uboreshaji wa huduma kutokana na watia saini kutoka katika jumuia ya watumia maji kutokubali kutoka katika kutia saini kwenye maswala ya kibank.
Post a Comment