Header Ads

MANISPAA MOROGORO YAIBUKA KINARA WA LISHE MKOA WA MOROGORO.



Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro, Ruth John akipokea cheti cha shukrani cha ushindi wa Manispaa ya Morogoro mara baada ya kuibuka kuwa kinara wa Lishe Mkoa wa Morogoro.(wapili kulia ) Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro. 

Mganga Mkuu Hospitali ya  Mkoa wa Morogoro, Dr. Musirye Ukio, akifuatilia kwa makini mkutano wa tathmini ya Lishe ya mfuko wa afya ya Jamii Mkoa wa Morogoro. 


Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba (kushoto) akipitia taarifa katika mkutano wa tathmini ya Lishe ya mfuko wa afya ya Jamii Mkoa wa Morogoro. (katikati) Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro Elina  Kweka, (kulia) Mchumi wa Manispaa ya Morogoro Jeremia Lubeleje.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro Enedy Mwanakatwe  (kulia) akifuatilia kwa makini mkutano wa tathmini ya Lishe ya mfuko wa afya ya Jamii Mkoa wa Morogoro. 

Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakiwa katika mkutano wa tathmini ya Lishe ya mfuko wa afya ya Jamii Mkoa wa Morogoro.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro leo Februari 03/2020 , imeibuka kuwa kinara wa lishe katika Mkoa wa Morogoro wakiwafuatiwa na Halmashauri ya Mvomero na Kilosa.

Akziungumza mara baada ya kupokea ushindi huo wa cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, mara baada ya kuibuka  kinara wa Lishe, Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro, Elina Kweka,amesema ushindi  huo umeifanya Manispaa hiyo kuanza kuongeza kasi zaidi ya kupambana na  changamoto za lishe duni kwa Watoto.

Kweka, amesema kuwa , watahakikisha kwamba wanaongeza uelewa na matokeo chanya kwa jamii ili kukabiliana na changamoto za afya na lishe zinazowakabili Watoto.

“Tumepokea cheti cha shukrani cha kuwa kinara wa hali ya lishe kimkoa, lakini ushindi huu umechangiwa na watu wengi , kwanza kabisa nimpongeze Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutenga fedha ambazo zimekuwa zikisaidia katika lishe,  Baraza la Madiwani la Manispaa , Mganga Mkuu wa Manispaa , Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa, wadau wa lishe, pamoja na  watoa huduma ngazi ya jamii na ngazi ya Vituo vya kutolea huduma, kwakweli wamefanya kazi kubwa  sana ya kuhakikisha Manispaa ya Morogoro inatokomeza watoto wenye udumavu, ombi langu endeleeni kupambana ikiwemo kutoa elimu mara kwa mara ili huduma hii iweze kutekelezeka vizuri katika Jamii”Amesema Kweka.


1 comment:

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.