DIWANI KANGA AKUTANA NA WADAU WA ELIMU
DIWANI wa Kata ya Kilakala Manispaa Morogoro, Mhe. Marco Kanga, amekutana na Wadau wa elimu kwa ajili ya kubadili maendeleo ya elimu katika Kata ya Kilakala.
Mkutano huo wa Wadau wa elimu umefanyika Februari 26/2021 katika Shule ya Sekondari Mazoezi Lupanga.
Akizungumza katika Mkutano huo, Mhe. Kanga ametawa wadau wa elimu kwa kushirikiana na Wazazi/walezi kuchangia katika elimu ili kuifanya Kata hiyo iwe na Wasomi wa kutosha wa kuweza kuleta maendeleo.
Kanga, amesema ni wakati Sasa Wazazi kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kutoa nguvu zao katika kuchangia maendeleo ya elimu ya Kata hiyo.
" Wanafunzi wengi wanafaulu, lakini changamoto ipo katika madarasa na madawati,nimoongeze Sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Sera ya elimu bila malipo, imefanya Wazazi kuamka na kuwapeleka Shule Watoto, jukumu letu Kama Wazazi tuchangie na sisi katika elimu ili kufanya viwango vya ufaulu kuongezeka kwa Watoto wetu" Amesema Kanga.
Aidha, amesema zipo changamoto nyiki katika Kata ya Kilakala ikiwamo huduma ya soko, Vituo vya afya, elimu, Miundombinu ya barabara lakini yote yatafanyiwa kazi kadri fedha zitakavyopatikana na Wadau wanavyojitokeza.
Mwisho amesema zipo Maabara ambazo hazijakamilika za muda mrefu ambazo kwa Sasa nguvu inahitajika ili kuweza kukamilika na kuzalisha Wanasayansi wengi na Wasomi Waziri katika kuleta maendeleo ya Kata na Taifa kwa ujumla.
Post a Comment