MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AGAWA VYAKULA NA BIMA ZA AFYA SHULENI, IFM WAMPA USHIRIKIANO
Mbunge wa Chalinze akishirikiana na Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaani IFM wamekabidhi Misaada mbalimbali zikiwemo Bima za Afya yaani CHF iliypboreshwa, vyakula, mavazi, vifaa vya kusomea na vitu mbalimbali kwa wananchi wa Chalinze na wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Lugoba.
Ikumbukwe kuwa ushirikiano huu baina ya Mbunge wa Chalinze na Wanafunzi wa Chuo hicho umeanza miaka miwili na wanafunzi hao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi zinazofanyika katika halmashauri hiyo.
Post a Comment