Header Ads

HALMASHAURI YA CHALINZE YAKABIDHI VITI -MWENDO 10 KWA WATOTO WENYE ULEMAVU KURAHISISHA USAFIRI SHULENI.


Halmashauri ya Chalinze leo imekabidhi Viti-Mwendo 10 vyenye kwa watoto wenye Ulemavu ili kuwawezesha wafikishwe shule. 

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo mheshimiwa Mbunge Ndg. Ridhiwani Kikwete aliwashukuru watendaji wa Halmashauri kwa utekelezaji wa maagizo yanayotolewa kwenye vikao. 

Mh. Kikwete, alipongeza hatua hii kuwa ni kubwa katika kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anakwenda Shule kama alivyoelekeza Mh. Rais  Daktari John Pombe Magufuli. Ndg. Kikwete alieleza furaha yake hasa kwa halmashauri kununua vifaa hivyo kwa kutumia mapato ya Ndani.

Kabla ya kukabidhi Ndg. Ramadhani Possi , mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze alimuhakikishia Mbunge kuwa Halmashauri imejipanga kujenga mabweni kwa ajili ya watoto hawa katika kata ya Kiwangwa na Bwilingu ili kuongeza ari ya kuhakikisha watoto wanasoma. Pamoja na hilo walimuomba Mbunge awasaidia kuongea na serikali ili lile ombi la kupata walimu wa ziada kwa ajili ya watoto hawa linafanikishwa kama walivyoahidiwa na Serikali.









No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.