Header Ads

MEYA KUMBILAMOTO AFANYA ZIARA SOKO KUU LA KISASA KISUTU ILALA.

 




Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto amefanya ziara yake ya kikazi katika Ujenzi wa Mabweni Shule ya Secondary ya Wavulana Azania. Lengo la ziara hiyo ni kufatilia maelekezo aliyoyatoa Feb 09 ya kumtaka Mkandarasi aongeze mafundi na speed ya kufanya kazi usiku na mchana ili Mabweni hayo yakamilike kwa wakati.


Mstahiki Meya amejionea ujenzi huwo na kuendelea kumsisitia Mkandarasi kuhakikisha Mabweni hayo yanakamilika kwa wakati na kuahidi kurudi tena.


Katika Ziara hiyo Mstahiki Meya aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azania Zungu pamoja na Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi.


Mwisho Mstahiki alitembea Ujenzi wa Soko la Kisutu ambapo kwasasa mafundi wanamalizia hatua za mwisho ikiwemo uwekaji wa namba katika Vizimba vya Soko hilo. Mwishoni mwa mwezi huu Wafanya Biashara wanatarajiwa kuingia katika Soko.


Aidha Soko hilo linatarajiwakutoa kipaumbele kwa wafanya Biashara wote ambao walikuwa wakifanya Biashara katika Soko hilo kwa ya Ujenzi.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.