RAIS MAGUFULI KUZINDUA SOKO LA KISASA MANISPAA MOROGORO LEO FEBRUARI 11/2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo Alhamisi Februari 11, 2021 anatarajia kuzindua soko la kisasa Morogoro na kisha kuzungumza na wafanyabiashara na wakazi wa Mkoa huo.
Uzinduzi huo utashuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, mkuu wa Mkoa huo, Loata Ole Sanare, wakuu wa wilaya za mkoa huo, wakurugenzi na wakuu wa taasisi mbalimbali.
Jengo la soko hilo la ghorofa moja lililogharimu Sh17.6 bilioni mpaka kukamilika lina maduka 304, vizimba 900, maeneo makubwa 16 kwa ajili ya taasisi za kibenki na ofisi, maegesho ya magari makubwa ya mizigo, maegesho ya magari madogo 143, vyoo, migahawa na stoo 36 za mitumba pamoja na bucha na maeneo ya kuchinjia kuku.
Mkandarasi wa ujenzi wa soko hilo ni kampuni ya Nandhra Engineering Construction.
Post a Comment