Header Ads

DIWANI KINGOLWIRA AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA ELIMU














DIWANI wa Kata ya Kingolwira,Mhe. Bidyagunze Mbaraka, amewata Wazazi wa Kata ya Kingolwira KUWEKEZA katika elimu ili kuwatengenezea Watoto wao maisha mazuri.

Kauli hiyo ameitoa Februari 06/2021, wakati akizungumza na Wazazi wa Watoto ambao hawajakamilisha  michango ya Madawati Shule ya Sekondari Kingolwira.

Bidyagunze, amesema huu ni muda ambao wazazi wanatakiwa kuanza kuwekeza nguvu kwa Watoto wao ikiwamo kuchangia michango ya Shule ambayo imepitishwa kisheria.

Amesema Kama wazazi wasipo kuwa mstari wa mbele kwa Watoto wao basi watakuwa wanajitengenezea kizazi ambacho hakina elimu lakini kushindwa kuwa na maarifa ya kujitegemea.

Aidha, amesema suala la Madawati ni agizo la Serikali  lililotolewa na  Waziri Mkuu , hivyo Wazazi lazima wawajibike kununulia Watoto Madawati.

" Niwaombe Wazazi tuwekeze Katika elimu, leo tunazungumzia Madawati, haipendezi Mtoto kukaa chini, hii ni adhabu hivyo Watoto hawa ili wafaulu vizuri lazima wakae katika mazingira rafiki Shuleni, utakuta Mtoto Shule ya Msingi amekaa chini, Sekondari akae chini hii siyo tu kusoma vizuri lakini pia Mtoto anaweza kupata ugonjwa wa mgongo, niwaombe haya tuliyokubaliana tuyatekeleze "Amesema Mhe. Bidyagunze.

Amesema kuwa lengo ni kutengeneza Kingolwira ya wasomi hivyo hakuwezi kupata wasomi Kama wazazi hawawekezi katika elimu.

Hata hivyo, amewataka Wananchi kuwabana Viongozi wao wa Mitaa kwani wao ndio wa kwanza Wenye dhamana ya kuwaletea maendeleo.

" Wananchi mnayo haki ya kuwabana Viongozi wenu wa Mitaa, hao wapo kwa ajili yenu na mnaweza kuuliza Mambo mengi huko Kuhusu maendeleo, lakini kila kitu mkinitupia Diwani Mimi nitawajibu lakini majibu yenu mengi mnapaswa muanzie huko kwa Wenyeviti wenu wa Mitaa ambao wao wanawasilisha taarifa zenu za Mitaa kwenye Baraza la Maendeleo ya Kata" Ameongeza Mhe. Bidyagunze.

Mwisho, amewataka Wananchi kushirikiana kwa pamoja na Viongozi wao waliowachaguw  kwani uchaguzi umeisha kinachotakiwa ni kutengeneza Kingolwira mpya na kuleta maendeleo kwa Wananchi.

Mkutano huo ambao aliuitisha Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kingolwira kwa kumualika Diwani kilijumuisha Wazazi wapatao 96 ambao Wana Watoto wa Kidato Cha kwanza wasio kamilisha michango ya Madawati Shuleni.





No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.