MNEC BANTU AWATAKA VIONGOZI WALIOCHAGULIWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ( NEC) ,Ndg. Hassan Bantu, amewataka Viongozi waliochaguliwa kushughulika na kero za Wananchi.
Hayo ameyazungumza leo Februari 06/2021 katika Maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM yalifanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwembesongo Manispaa Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema uchaguzi imeisha hivyo jukumu la Viongozi ni kuwatumikia Wananchi waliowachagua.
Bantu, amesema kuwa, Wanachama wamewaamini Sana hivyo ili kujenga imani zaidi na Chama ni kuwatumikia na kutatua kero zao.
Amesema kuwa muelekeo wa Chama ni kuongeza idadi ya Wanachama, hivyo Wananchi watakuwa na imani zaidi endapo yale wanayoyatarajia yatafanyiwa kazi.
Hata hivyo, amewataka Viongozi kuitisha Mikutano ya kisheria ili kuendelea kuleta maendeleo katika maeneo yao ya kiutawala.
Pia amewataka Viongozi wa Chama kuhakikisha wanapiga vita dhidi ya rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.
" Shughulikeni na matatizo ya Wananchi, mmeaminiwa, kwahiyo hakikisheni mnayenga muda wenu wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wenu"Amesema Bantu.
Hata hivyo, amewataka Wana CCM wajenge utaratibu wa kuvaa sare ili wanapokuwa katika vikao vyao waweze kujitofautisha na vikao nyengine.
Mwisho, amewapongeza Sana Wana CCM kwa kumpatia kura nyingi Sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwa na kura nyingi , hususani Manispaa Morogoro kwa kumpa Rais kura asilimia 99.
Post a Comment