Header Ads

WAFANYABIASHARA SOKO KUU MANISPAA YA MOROGORO WAPONGEZA UJENZI WA SOKO, WAAHIDI USHIRIKIANO KULINDA MIUNDOMBINU


Soko Kuu la Manispaa Morogoro.


Mfanyabiashara.
Mfanyabiashara.
Meneja wa Soko Kuu la Kisasa Manispaa Morogoro,Alatutosia Sanga , akizungumza juu ya Soko hilo.

Bidhaa zilizopo Sokoni.

WAFANYABIASHARA Soko Kuu la Manispaa ya Morogoro, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk John Magufuli, kwa kutoa fedha Sh bilioni 17.6 zilizowezesha kujengwa soko jipya la kisasa lenye ghorofa moja huku wakiaahdii kutoa ushirikiano kuhakikisha wanalinda miundombinu ya Soko hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti leo Februari 9/2021, wamesema Tangia Soko hilo lifunguliewe Januari 01/2021, ,umefanya waweze kufanya  kazi katika mazingira rafiki licha ya changamoto za hapa na pale.

Akizungumza juu ya Ujenzi huo, Mfanyabiashara Saidi Ramadhani,amesema kuwa Soko hilo limekuwa na tija sana kwani limeweze kuwaboreshea mazingira mazuri ya kufanyia kazi tofauti na Soko la zamani ambalo halikuwa na miundombinu  rafiki kwa wafanyabiashara.

Habiba Shabani ambaye pia ni mfanyabiashara wa Soko hilo, amempongeza Mhe. Rais kwa kuipatia fedha  nyingi katika kipindi cha miaka mitano  ya uongozi wa Rais Dk Magufuli.

Naye Meneja wa Soko Kuu la Manispaa Morogoro Alatutosia Sanga,  ya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ameendelea kumshukuru Rais na kusema, ujenzi wa soko hilo huku akisema kuwa Soko hilo ni miongoni mwa miradi endelevu itakayoiingizia halmashauri mapato yatakayosaidia kuboresha huduma za kijamii.

“ Kwa muda mfupi wa uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, tumepata fedha nyingi za maendeleo , ujenzi wa soko kuu jipya , pia kuwezesha stendi ya mabasi ya Msamvu kurudi mikonini mwa Manispaa , haya ni mafanikio makubwa na tunampongeza na kumwombea maisha marefu, lakini pia Mkurugenzi wetu amekuwa karibu sana kufuatilia kero za Wafanyabiashara kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya na Mkoa ” Amesema Sanga.

Hata hivyo , amesema walizingatia makubaliano ya  wafanyabiashara  waliokuwa soko la zamani kabla ya kuvunjwa kupisha ujenzi huo, ambapo wao waliweze kutoa kipaumbele kuwapatia Vizimba vya biashara.

“ Ujenzi wa soko hili mara baada ya kukamilika , tulitekeleza makubaliano kwa wafanyabiashara wetu  kwamba wao tutawapa vipaumbele kuingia hapa, ambapo kabla ya ujenzi wafanyabiashara hao wapatoa zaidi ya 900 tumuewapeleka kwa muda soko la Manzese pamoja na maeneo mengine ya kutolea huduma, hivyo Soko letu kwa sasa limejaa  na Wafanyabiashara wote tumewapatia Vizimba pamoja na Maduka na Soko linaendelea kufanya kazi licha ya changamoto za hapa na pale ambazo Uongozi unazifanyia kazi maana maendeleo yoyote ynakuwa na changamoto zake" Ameongeza Sanga.

Soko hilo lilijengwa  baada ya Wizara ya fedha kupitia Hazina kuipatia halmashauri hiyo , kiasi cha fedha hizo baada ya soko la zamani iliyojengwa mwaka 1953 kuwa chakavu na kuvunjwa .


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.