WAZAZI WAASWA KUTOA MALEZI BORA KWA WATOTO ILI KUTIMIZA NDOTO ZAO.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidna Mathias, akizungumza na Washiriki katika Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia .
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidna Mathias,akisalimiana na Watoto kutoka Makao ya Multi Dome Relief Centre mara baada ya kuhitimisha kilele hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii, Joyce Mugambi, akizungumza na Washiriki katika Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia .
Mwakilishi wa Dawati la Kijinsia Polisi Kituo Kikubwa Morogoro, Mariam Masalu,akizungumza na Washiriki katika Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia .
Afisa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Bigambo Thomas,akizungumza na Washiriki katika Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia .
Afisa Ustawi wa Jamii ,Hamisa Kagambo, akizungumza na Washiriki katika Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia .
Afisa Ustawi wa Jamii, Luluvilo Lulanda, akitoka kutunza wasanii waliotumbuiza katika kilele hicho cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Vita ukatili wa Kijinsia.
Maafisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro .
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Sidna Mathias, (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Makao ya Watoto ya Multi Dome Relief Centre, Ndug. Fauzi Karama Jumaa( wapili kutoka kulia) mara baada ya kuhitimisha kilele cha Siku 16 za kupinga Vita Ukatili wa Kijinsia.
Maafisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Makao ya Watoto ya Multi Dome Relief Centre,mara baada ya kuhitimisha kilele cha Siku 16 za kupinga Vita Ukatili wa Kijinsia.
WAZAZI wameaswa kuchukua hatua madhubuti ya kuhakikisha kwamba Watoto wanapatiwa malezi bora na mahitaji yao muhimu ili waweze kutimiza malengo yao na kufikia ndoto zao.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ,Sidna Mathias, katika kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vita Ukatili wa Kijinsia ambapo Manispaa ya Morogoro iliadhimisha katika Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Kihonda leo Desemba 10/2020.
Akizungumza na Washiriki katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sidna, amesema kuwa suala la Ulinzi na Usalama wa Watoto sio suala la Serikali pekee bali ni suala la kila mzazi kuhakikisha ulinzi na Usalama wa Watoto unazingatiwa .
“Leo tuna hitimisha kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia , niwaase wataalamu waendelee kutoa elimu hii ya ukatili wa Kijinsia ili tuweze kupunguza au kutokomeza kabisa matukio ya ukatili katika Jamii yetu, lakini tujitahidi ndugu zangu kufichua matendo yote ya ukatili na taarifa zetu tuzitoe kwa siri ili wale wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za Kisheria ” Amesema Sidna.
Sidna, amesema lengo la maadhimisho hayo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa Jamii juu ya ukatili na madhara yake hususani kwa Wanawake na Watoto pamoja na jinsi ya kuzuia ukatili wa Kijinsia usiendelee kuwa janga miongoni mwa Jamii.
Aidha,amesema Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo, CVM, Boresha Afya, Morogoro Parallegal na Polisi Dawati la Jinsia katika kuelekea kilele hicho imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali zikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii juu ya ukatili wa Kijinsia kupitia Redio ya Dizzim, Redio ya Abood, MVIWATA , utoaji elimu Shuleni pamoja na midahalo mbalimbali ya kujadili juu ya ukatili wa kijinsia kwa Wanajamii katika Kata mbalimbali ikiwemo Kata ya Kichangani, K/Ndege, Lukobe na Mwembesongo.
Mwisho amechukua fursa ya kutoa shukrani kwa Wazazi , Dawati la Jinsia Polisi Kituo Kikubwa, Wamiliki wa Makao na Vituo vya Watoto wadogo, Wananchi na Watoto wote waliohudhuria katika kuhitimisha Kilele hicho cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Kwa upande wa Mtoaji maada kutoka Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro, Hamisa Kagambo, amesema wamekuwa wakishuhudia kupokea taarifa juu ya ukatili wa kimwili na kingono kwa Watoto wa kike pamoja na Wanake jambo ambalo amesema ipo haja kubwa ya jamii kupatiwa elimu ili kutokomeza vitendo hivyo.
Amesema , Manispaa ya Morogoro kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii, imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara kwa jamii juu ya ukatili wa Kijinsia.
Kwa upande wa Afisa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro, Bigambo Thomas, amesema sababu kubwa inayopelekea ukatili wa Kijinsia ni pamoja na mmomonyoko wa maadili , hali ambayo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika Jamii.
Bigambo,amesema kuwa katika Ukatili wa kingono waathirika wakubwa wa matukio hayo ni pamoja na Wanawake,Watoto na Wanafunzi , hivyo ametoa rai kwa Wazazi kukaa na Watoto wao ili kuangalia mienendo yao kwani vipo vitendo wanafanyiwa lakini wamekuwa wasiri sana kuvielezea.
Naye, Mwakilishi wa Dawati la Kijinsia Polisi Kituo Kikubwa Morogoro, Mariam Masalu , amesema watu wanapofanyiwa ukatili wanatakiwa kukimbilia katika Dawati ili hatua ziweze kuchukuliwa kwani bila kufanya hivyo na kujichukulia maamuzi yao wanapoteza ushahidi.
Ikumbukwe kwamba Maadhimisho hayo yameratibiwa na Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na wadau wa CVM ambao wamekuwa wadau wakubwa wa Manispaa ya Morogoro katika kupinga vita ukatili wa Kijinsia pamoja na kutetea haki za Wafanyakazi wa Nyumbani ambao wamekuwa wakiwawezesha katika kufikia ndoto zao.
Post a Comment