DIWANI KILAKALA AWATAKA VIJANA KUTUMIA MICHEZO KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO.
DIWANI wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amewahimiza vijana Kata ya Kilakala kutumia michezo ili kuimarisha amani, upendo na mshikamano.
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 04/2020 kwenye Uwanja wa kwa Winga Kilakala , wakati wa hafla fupi ya pongezi ya timu ya Mpira wa Miguu ,Nughutu FC , baada ya kuibuka kidedea katika fainali ya mashindano ya Jezi yaliyofanyika Novemba 29/2020 katika Viwanja vya Sabasaba.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, ambapo Vijana
walikusanyika kwa lengo la kushiriki katika hafla hiyo ,Kanga , ameeleza kuwa michezo imekuwa ikitumika kwa
kiasi kikubwa katika kuimarisha ushirikiano na kuwajengea vijana uzalendo.
“Kupitia michezo mnayofursa kama vijana
kuendelea kuenzi falsafa za waasisi wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na
Hayati Mzee Abeid Amani Karume ambao walikuwa wazalendo kwa taifa lao na
waliimarisha muungano kwa maslahi ya watanzania wote, niwatoe hofu nitasimama
bega kwa bega na nyinyi katika kuhakikisha michezo katika Kata yetu inakuwa
namba moja, mlionenyesha imani na mimi mkanipatia ridhaa ya kuwa Diwani wenu,
basi mimi nitatekeleza kwa vitendo ,” Amesema Kanga.
Kanga,
amesema kuwa michezo hiyo
iliyowakutaisha vijana ikatumike kama sehemu ya kuwa na amani, uvumilivu na
mshikamano.
“Hiki
mlichokifanya kimeleta fahari sana katika Kata yetu, nimpongeze sana Mwenyekiti
wa Mtaa wa Nughutu ,amefanya kazi kubwa sana ya kujitoa na kupata ushindi,
lakini sitowasahau wadau mbalimbali ambao walikuwa pamoja nasi katika kufanikisha
timu yetu inafanikiwa kuchukua ubingwa, kikubwa mtambue kwamba Vijana mnatakiwa
kujenga taifa kwa vitendo vinavyodumisha amani, upendo na mshikamano kama ambavyo
Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere alivyotujengea taifa lenye umoja,”
Ameongeza Kanga
Aidha , amewasihi vijana kutambua wajibu wao katika
jamii na kuifanya michezo kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu wanayopaswa
kuyaendeleza katika kutekeleza mipango waliyonayo.
Katika
hatua nyengine, Kanga, ametoa kiasi cha Shilingi 200,000/= kwa ajili ya kuwapa
motisha Vijana kuendelea kujituma zaidi
na kuiletea heshima Kata ya Kilakala katika Nyanja za michezo.
Mbali
na fedha, pia ameahidi kuikabidhi timu hiyo mbuzi 2 katika kikao cha wadau kitakachofanyika
siku za usoni ikiwa ni zawadi kwa niaba ya Ofisi ya Kata, Ofisi ya Chama pamoja
na Wananchi wa Kilakala.
Hata
hivyo, amewataka na kuhimiza Vijana kuunda vikundi kwa ajili ya kupatiwa mikopo ya
Halmashauri inayotolewa ya asilimia 10 huku gharama za usajili akiahidi
kuzibeba yeye.
Mwisho,
amesema kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, yupo mbioni kuanzisha Kombe la Kanga
CUP, litakaloshirikisha timu za mitaa yote ndani ya Kata ya Kilakala ambapo
washidni watapewa zawaidi kubwa kabambe ambayo bado imekuwa ni siri mpaka pale
mashindano yatakapo tarajia kuanza.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Kata ya
Kilakala, Scolastica Mwanyika, amesema
kuwa michezo imekuwa na umuhimu wake ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaendeleza vijana
ili waweze kuimarika kiafya na kiakili.
“Michezo ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) , hivyo kwa kutambua hilo sisi Viongozi wa Chama kwa
kushirikiana na Viongozi wa Serikali , tutakuwa bega kwa bega katika kuinua viwango vya michezo, lakini
niwaombe tuzitumie hizi nafasi kwani michezo kwa sasa ni ajira kama zilivyo
ajira nyengine, lakini kikubwa zaidi tusijihusishe na vitendo vya uharaifu
kwani vitatusababishia kuharibu mfumo wa maisha yetu kwa kupoteza maisha au
kuishia jela””Amesema Scolastica.
Mwisho , amesema yupo tayari kuchangia
kuhakikihsa kwamba Kata ya Kilakala inakuwa vinara katika michezo mbalimbali
Manispaa ya Morogoro.
Naye Mtendaji wa Kata ya Kilakala, Amina Said, ameahidi kuwapatia Vijana hao mipira katika kukabiliana na changamoto ya mipira wanayokumbana nayo hivi sasa.
Post a Comment