Header Ads

Mganga mkuu Manispaa Morogoro awaonya wamiliki wa Zahanati zisizo zingatia sheria.





 MGANGA Mkuu wa Manispaa Morogoro, Dr Ikaji Rashidi, amewaonya wamiliki wa Zahanati za afya ambao zimekuwa zikiendesha huduma  bila kuzingatia sheria hususani katika suala zima la usajili.

Kauli hiyo ameito Desemba22/2020 wakati wa ziara ya kukagua Zahanati  zinazomilikiwa  na watu binafsi.

 Akizungumza Kuhusu Zahanati hizo amewataka Wamiliki wa Zahanati zote ambazo hazijasajiliwa wafike Ofisi Kuu ya Mganga wa Manispaa  kwa ajili ya kupata usajili  kabla ya yeye kuchukua hatua Kali ya kisheria. Dr Ikaji amesema Wananchi wamekuwa wakiwaamini Sana Wataalamu hao lakini huduma inayotolewa hazingatii afya ya mteja. Amesema katika ziara yake amebaini kuwa Zahanati nyingi zimekuwa zikitoa huduma bila kuzingatia usajili Jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Sheria za afya. " Nimefanya ziara hii baada ya kubaini Kuna Changamoto katika Zahanati hizi zinazomilikiwa na watu binafsi, lakini wamekuwa wakitoa huduma bila usajili, niombe wamiliki wote wafike Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa kwa ajili ya kupatiwa usajili, sisi tunaziara kubwa ya Kimkakati tunaendelea kubaini Zahanati  ambazo zimekuwa zikiendesha huduma za afya kwa  vunja sheria, tufanyeni kazi kwa kuzingatia sheria, tunawatibu binadamu lazima tuzingatie Taaluma zetu, Kama umeshindwa kusajili, funga sio lazima utoe hii huduma " Amesema Dr Ikaji. Amesema kuwa miongoni mwa changamoto alizokumbana nazo ni pamoja na Darubini kutofanya kazi, hakuna chombo Cha kusafishia vifaa vya maabara, stoo za dawa kutumika Kama duka la dawa, Mazingira mabovu ya miundombinu pamoja na Maeneo ya kuhifadhia taka. 

Mwisho, amewataka Wamiliki wote wa Zahanati wazisajili ili waweze kutoa huduma Bora kwa wananchi kwa kuzingatia sheria na kanuni za afya.

Miongoni mwa Zahanati zilizofungiwa  kutokana na makosa Ni pamoja na Zahanati ya BMG kata ya Mafiga, Maabara ya ijue afya yako.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.