ZOEZI LA UHAKIKI REJEA WALENGWA WA MPANGO WA TASAF MANISPAA YA MOROGORO KIPINDI CHA PILI AWAMU YA TATU KUANZA KESHO DESEMBA 08/2020.
Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini TASAF Makao Makuu, Farig Michael,(kushoto), Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana (katikati) , Afisa TAMISEMI, Idrisa Mtandi wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandikishaji mara baada ya kumalizika kwa mafunzo leo Desemba 07/2020 katika Ukumbi wa Msamvu Manispaa ya Morogoro.
ZOEZI la Uhakiki rejea wa Kaya zilizopo katika Mpango wa TASAF Manispaa ya Morogoro kuanza kesho Desemba 08/2020 .
Kauli hiyo imetolewa na Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini TASAF Makao Makuu, Farig Michael, leo Desemba 07/2020 katika Ukumbi mdogo wa Msamvu wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji
Akizungumza juu za zoezi hilo, Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini TASAF Makao Makuu, Farig Michael, amesema kuwa zoezi hilo litaendeshwa kwa Kaya ambazo hazikufanya uhakiki katika kipindi cha kwanza awamu ya tatu awamu ya tatu kutokana na sababu mbalimbali.
Farig,amesema kuwa, Mkazo mkubwa katika Kipindi cha Pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato na kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na afya.
Amewasisitiza Viongozi na Maafisa Waandikishaji Kaya kufanya kazi kwa uadilifu na weredi wakati wa utekelezaji wa Zoezi hili kama maagizo yaliivyotolewa na Mh Rais katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili kuhusu uwepo wa kaya hewa.
Aidha, amesema kuwa Uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu ni muhimu katika kusimamia zoezi la uhakiki wa Walengwa wa Mpango wa TASAF ambao utasaidia kupata Takwimu sahihi za wanufaika Halisi ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Naye, Mratibu wa TASAF, Manispaa ya Morogoro, amesema wnaatarajia zoezi hilo kuanza kesho Desemba 08/2020 ambapo litachukua muda wa siku nne kukamilika.
"Leo tupo hapa kwenye mafunzo kwa ajili ya kufanya uhakiki rejea ambao tunaanza kesho Desemba 08/2020, lakini walengwa hawa sio wapya bali ni wale waliopo katika malipo wa awamu ya kwanza tulioanza mwezi wa 7/2020 ambao hawaja hakikiwa kutokana na sababu mbali mbali, kwa hiyo Serikali imeandaa utaratibu mwengine wa kuwafikia ambapo Maafisa Watendaji wote wa Kata watawataarifu wale walengwa ambao hawaja hakikiwa " Amesema Katema.
Kata ambazo zitahusika na mpango huo wa uhakiki rejea ni pamoja na Bigwa, Chamwino, Kauzeni, Mafiga, Kiwanja cha Ndege, Kichangani, Magadu, Kihonda, Kihonda Maghorofani, Kilakala, Kingo , Kingolwira, Mazimbu , Luhungo pamoja na Kata ya Lukobe.
Post a Comment