Header Ads

Diwani mteule Kata ya Kilakala awashukuru wananchi.

Diwani Mteule Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya kutoa shukrani kwa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Wananchi wa Kata ya Kilakala kwa kupata kura za kishindo. 









Katibu wa Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini, Peter Mwema, akizungumza kwa ajili ya kuwashukuru Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa kukiamini chama hicho kuendelea kushika Dola .


Diwani mteule wa Kata ya Kilakala, Marco Kanga,  amewashukuru wananchi wa Kata ya Kilakala  kwa kumchagua kuwa diwani wa kata hiyo.

Kanga, amewapongeza wananchi wake pamoja na kufanya ziara ya kutatua kero Kata ya Kilakala ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake ambao amejiwekea katika kusikiliza kero za Wananchi ndani ya kata hiyo.

“Tumefanya uchaguzi wa kihistoria na Kilakala imeonyesha mfano , siwezi kutumia nafasi mliyonipa kwa kusaka umaarufu binafsi na mali ambao hawajanipigia kura wamenipa nafasi ya kuwadhihirishia kwamba mimi ni bora na wakati ujao wataniunga mkono, nawashukuru wanachi wangu kwa kunichagua na kwa ushindi mnono kwa Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia kura za Mbunge Mhe. Abdulaziz Abood,  Rais John Magufuli na Diwani. Amesema Kanga.

Kanga,  amewashukuru wananchi wake wa eneo la Kilakala  kwa kumpa ridhaa kushika dola kwa kipindi hichi cha uongozi wake na kuwataka washirikiane pamoja katika kuijenga Kilakala ya Kisasa.

Hata hivyo amesema katika uongozi wake amejipanga kutatua kero mbalimbali atasimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kutekeleza yale yote yalioainishwa kwa mwaka 2025 .

Kwa Upande wake, Katibu wa Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini, Peter Mwema,  amewashukuru wananchi wa Kata ya Kilakala na Jimbo la Morogoro Mjini kwa  kukiamini Cha Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukipa madiwani wote wa kata 29 na Mbunge na kwamba sasa kazi iliyobakia ni kuhakikisha wateule hao wanatekeleza ilani ya chama hicho kwa vitendo kama walivyoahidi.

Naye Mwenyekiti  U.W.T Wilaya ya Morogoro Mjini, Victoria Saduka , akizungumza na  wananchi wa Kata ya Kilakala,  amewashukuru wananchi kwa kuendelea kuiamiani CCM na kuchagua wagombea wote.

"Morogoro Mjini  fora, hususani Kata ya Kilakala  , asanteni sana kwa kuchagua Madiwani wote wa CCM, Mbunge wa CCM na Rais wa CCM , kazi iliyombele yetu ni kuhakikisha tunakwenda kuitekeleza Ilani kwa kishindo kama mlivyo kiamini chama bila upendeleo wa aina yoyote" Amesema Mama Saduka .

Katika hatua nyngine, Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilakala kimewazawadia vyeti watu waliojitolea kwa hali na mali katika ku fanikisha zoezi hilo la Uchaguzi licha ya watu wote kuwa muhimu lakini wapo ambao walijitolea kwa hali na mali kuhakikisha CCM kilakala inapata ushindi.





No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.