Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO WAANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA SERIKALI LA UJENZI WA SHULE MPYA ZA SEKONDARI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba (katikati) akipokea maelezo ya taarifa ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari  kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu (kulia).



Eneo linalotarajiwa kujengwa shule mpya ya Sekondari lililopo Kata ya Boma.




MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amefanya ziara akiambatana na Wajumbe wa CMT katika kukagua eneo la Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari inayotarajiwa kujengwa katika Kata ya Boma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali kupitia maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Akizungumza juu ya Ujenzi wa shule hiyo, Lukuba, amesema kimsingi Ujenzi wa Sekondari hiyo unakwenda kupunguza changamoto ya Wanafunzi kusafiri umbali mrefu wa kwenda na kurudi shuleni.

Lukuba, amesema mafanikio ya mradi huo yapo kwenye mikono ya Wananchi na iwapo mradi huo utakwama nao utakuwa umewakwamisha.

"Tumetafuta eneo hili kutokana na maelekezo ya Serikali ya kila Halmashauri kuwa na Shule mpya ya Sekondari, tumeona tukimbie kwa kasi ya ajabu tuhakikishe agizo hili tunalianza mapema iwezekanavyo,jambo hili litakapoanza litakuwa shirikishi , hivyo ni vema tukaanza pamoja na kumaliza pamoja niwaombe Wananchi tuendelee kuhamasishana katika ujenzi wa madarasa ili watoto wetu waliofaulu waweze kuingia darasani" Amesema Lukuba.

Manispaa ya Morogoro katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu 2020 , imefaulisha jumla ya wanafunzi 7577 ambapo kati ya hao wasichana 3927, wavulana 3650 sawa na asilimia 90.22% ya wanafunzi wote waliofaulu.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.