Header Ads

MHE. ABOOD AVISHAURI VYOMBO VYA HABARI HAPA NCHINI KUUPA KIPAUMBELE MCHEZO WA WAVU.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, akisalimiana na Wanamichezo wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo katika Uwanja wa UMWEMA Bwalo la JKT Manispaa ya Morogoro.







MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amevishauri vyombo vya habari hapa nchini  kutoa kipaumbele kwenye michezo mwingine ikiwemo mchezo wa mpira wa wavu kwani kufanya hivyo kutaleta hamasa  kwa jamii kuipenda pamoja nakufungua ajira kwa vijana wengine tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo imetolewa Desemba 02/2020 na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe.Abdulaziz Abood, akifungua Mashindano ya  Klabu Bingwa ya Taifa 2020 ya mpira wa wavu Tanzania bara yanayoendelea kufanyika katika Uwanja wa Bwalo la UMWEMA  JKT Manispaa ya Morogoro.

Abood, amesema yeye kukubali kuwa mlezi wa chama hicho atahakikisha mchezo huo unatangazwa nakuhamasishwa ipasavyo kwenye vyombo vya habari hapa nchini ikiwemo kuwashirikisha wadau wengine kuwekeza kikamilifu ili kurudisha mchezo huo kwenye jamii nakueleza kuwa hata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  chini ya Mwenyekiti wake Dk John Pombe Magufuli inaeleza vizuri namna michezo itakavyoendelezwa nakusimamiwa na Rais mwenyewe ni mpenda michezo na muda wote amekuwa mstari wa mbele kwa wanamichezo wote.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TAVA  Taifa Meja Jenerali Mstaafu Patrick Mlowezi, amesema Mashindano hayo yanajumuisha wadau kutoka Mikoa mbali mbali.

Amesema miongoni mwa mafanikio wanayotarajia kuyapata katika mashindano hayo ni pamoja na  kuibua vipaji,kuendelea na kuimarisha viwango vya uchezeshaji wa wachezaji pamoja viwango vya uamuzi kwa waamuzi nchini,kusaidia upatikanaji wa nafasi za kazi,kuzuia tabia hatarishi katika jamii,kumchagua wachezaji wa timu ya Taifa kea upande wa Tanzania bara,kuendeleza na kuimarisha umoja na mashindano kwa wadau wa mchezo huu na Taifa kwa ujumla kwani inajumuisha wadau toka mikoa mbalimbali.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.