Header Ads

MBUNGE CHALINZE ASEMA SHIDA YA MAJI KIBINDU KUWA HISTORIA


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, akizungumza juu ya ufumbuzi wa shida ya maji.








MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete,  amewahakikishia wananchi wa Kata ya Kibindu kuwa shida ya maji  itabaki kuwa historia.

 Akiongea mbele ya wananchi wa Kijiji cha Kwamduma, kata ya Kibindu Mh.Mbunge alimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali ya awamu ya tano kwa hatua zinazochukuliwa kupata ufumbuzi wa shida ya maji katika kata hiyo.


Maneno hayo aliyatoa katika Mkutano huo wa wananchi uliohudhuriwa pia na wataalamu mbalimbali toka taasisi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Kawawa. 

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya , Mh.Mbunge amemshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya Mh. Raisi kwa hatua zilizokwisha fikiwa. Vilevile Mh. Mbunge alieleza kuridhishwa kwake na hatua mbalimbali zilizochukuliwa. 

Kwa upande wake alieleza kuwa yeye kama Mbunge amefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuchimbwa kwa visima zaidi ya vinne katika vijiji mbalimbali vya kata hiyo ikiwemo Kwamduma visima viwili, kibindu viwili, na Kwamsanja kimoja ambavyo vimesaidia kidogo japo shida bado haijaisha.

 Alishukuru serikali kwa hatua zinazochukuliwa sasa alisema,"...Uchimbaji wa mabwawa haya makubwa na usambazaji kwenda kwa wananchi unakuja wakati muafaka, hivyo matarajio ni kwenda kutatua shida ya Maji kwa ukubwa huo uliokusudiwa. Kwa hakika tuna kiongozi ambaye sio anasema  mdomoni kuwajali wananchi wanyonge isipokuwa anatenda kwa vitendo pia."


Akizungumza mbele ya wananchi kijiji Kwamduma,Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Kawawa, alieleza kuwa Serikali imejidhatiti kuhakikisha maji yanawafikia wananchi wa Kibindu hivyo alimuhakikishia Mbunge na wananchi kuwa mradi utakamilika mapema ili wananchi wapate maji safi na salama. 

Akieleza juu ya Utekelezwaji wa miradi hiyo Mkuu wa Wilaya huyo alieleza kuwa, tayari Serikali imetoa Bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi yote ikiwemo Milioni 700 kwa ajili ya Kwamsanja na Milioni 900 kwa ajili ya Mjembe, Kwamsanja ambayo inatarajiwa kwa pamoja kutoa lita zisizo pungua Milioni Tatu na Nusu. Wingi ambao unakwenda kutatua kero ya Maji katika kata ya Kibindu.

Miradi hiyo itakapokamilika inataraji kuhudumia watu wanaoishi katika eneo la Kibindu na vitongoji vya kata za Jirani.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.