Header Ads

DC MSULWA, AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KATIKA KAMPENI YA KUPANDA MICHE YA MITI 15000 PEMBEZONI MWA BWAWA LA MINDU MANISPAA YA MOROGORO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akipanda mche wa mti kuashiria uzinduzi rasmi wa Kampeni ya upandaji wa miti pembezoni mwa Bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro leo Desemba 09/2020.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika Kampeni ya upandaji wa miti Mto Mindu.

Bregedia Jenerali, Seif Hamisi akipanda mti.
Mkurugenzi wa MORUWASA, Eng. Tamim Katakweba, akipanda mti.

         
Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar , Ndug. Abdurahman Milao akipanda mti.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, akipanda mti.

Mwanafunzi akishiriki katika zoezi la upandaji wa miti.
            
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akizungumza na wananchi walioshiriki katika Kampeni ya upandaji wa miti.

      

Mkurugenzi MORUWASA, Eng. Tamim Katakweba, akizungumza na hadhara ya wananchi waliojitokeza katika Kampeni ya upandaji wa miti.
  

         
          

MKUU wa Wilaya ya Morogoro. Mhe. Bakari Msulwa, ameongoza mamia ya Wananchi wa Manispaa ya Morogoro ikiwamo Taasisi za Serikali na za watu binafsi kushiriki katika Kampeni ya Kupanda Miche ya Miti 150000 pembezoni mwa Bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro .

Zoezi hilo la Kampeni ya upandaji wa Miti pembezoni mwa Bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro  limefanyika leo Desemba 09/2020 ikiwa ni Sherehe ya kutimiza miaka 59 ya Uhuru wa Tanzania.

Akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi walioshiriki katika zoezi hilo, DC Msulwa, amesema kuna umuhimu mkubwa na faida nyingi katika utunzaji wa mazingira hususani kupanda miti pembezoni mwa Mito na Mabwawa ambapo faida zake ni pamoja na kupata hewa safi, mvua za kutosha , kivuli, kutumika kama mipaka na kulinda vyanzo vya maji .

Aidha, amesema katika Siku ya leo , Wilaya yake ikiwamo Halmashauri zote mbili zimeandaa kampeni hiyo ya kupanda miti ili kulinda vyanzo vyake vya maji na kuendelea kutoa huduma bora ya Maji kwa Wananchi.

“Nimefurahishwa sana na Kampeni hii, kwani vyanzo vyetu vya maji hali tete watu wanafanya shghuli za kiuchumi katika vyanzo hivyo, wengine wanaziba vyanzo, sasa nimeambiwa Bwawa letu lina miaka 40, unafikiri kama tungeanza uharibifu nyuma tungekuwaje? Niwaombe tuache shghuli katika vyanzo vya maji, Bwawa lina jaa matope , tumeanza naomba wale wenye mashamba tuliyopanda miti watusaidie kusimamia miti hiyo ikue, ugomvi wetu utaanza hapa haiwezekani mazao yako yanakuwa na miti yetu inakufa wakati ipo katika shamba lake, nitoe wito tusiishie hapa kila mtu anawajibu wa kulinda vyanzo vya maji ili tuendelee kupata huduma hii” Amesema DC Msulwa.

“”Pamoja na yote, nimefurahishwa sana na ujio wa wageni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar, hii imeonyesha ni jinsi gani Muungano wetu ulivyo na thamani kubwa ndani ya Taifa hili, tunaomba tuuenzi Muungano wetu kwani unafaida kubwa sana kwa Taifa letu na Maendeleo yetu “ Ameongeza DC Msulwa.

Katika hatua nyengine, DC Msulwa, ametoa wito kwa Wazazi kuhakikisha ifikapo mwakani  kila mzazi anapomwandishikisha mototo na wale wanaaonza kidato cha kwanza kufika shuleni hapo akiwa na mche mmoja wa mti ili kuweka mazingira yenye ukijani.

Kwa upande wa Brigedia Jenerali , Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la  Mazao Kikosi cha Mzinga, Seif Hamisi, amewaasa washiriki na wananchi kujali mazingira ya sehemu wanazofanyia kazi na kuahidi kuwa miti hiyo iliyopandwa itatunzwa na kulindwa ipasavyo kwa kushirikiana na Uongozi na Wananchi wa eneo la Bwawa la Mindu ambapo ndipo Kambi ya Mzinga ilipo.

"Tunataka Kampeni hii ya upandaji wa miti iwe endelevu ili kuhakikisha Mindu inapokea maji mengi kutoka katika vyanzo vya maji pamoja na kurudisha Mindu katika ukijani wake  unaotakiwa kwani  Mindu ya Kijani inawezekana" Amesema Brigedia Jenerali Seif.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema Manispaa ya Morogoro haipo nyuma ambapo wana wadau ambao wameingia nao mkataba wa kila mwaka kuwapatia miche kwa ajili ya kupanda.

Waluse, amesema Ofisi ya Manispaa ipo wazi inashirikiana na wadau wote wa Mazingira ikiwa na lengo la kuweka Mji safi lakini kutunza vyanzo vya maji visiweze kuharibiwa kutokana na shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wananchi.

“ Kwa upande wetu Manispaa ya Morogoro, tunakusudia kupanda miti mingi kwani licha ya kuwa ni agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu pia ni faida kwa vizazi vijavyo” Amesema Waluse.

Naye, Mkurugenzi wa MORUWASA Manispaa ya Morogoro, Mhandisi  Tamim Katakweba, amemshukuru Mkuu wa Wilaya Mhe. Bakari Msulwa pamoja na Bregedia Jenerali ,Seif Hamisi ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Jeshi  Mazao Mzinga , kwa kukubali kuhudhuria uzinduzi huo wa Kampeni ya kupanda miti ambapo awamu ya kwanza imepandwa miche ya miti 15000 kati ya miche ya miti ya miche 500000 iliyopangwa kupandwa katika eneo hilo la pembezoni mwa Bwawa la Mindu.

“”Leo tumeshuhudia Mkuu wetu wa Wilaya akiongoza Kampeni ya upandaji wa Miti, viongozi na wnanachi wamepanda miti ikiwa ni uzinduzi wa Kampeni ya upandaji wa miti katika Vyanzo vya Maji Wilaya ya Morogoro inayosimamia na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Ofisi ya Bonde la Mto Ruvu, Ofisi ya Idara ya Misitu pamoja na sisi watu wa MORUWASA, niendelee kuchukua nafasi hii kuwaomba wale wakazi wanaofanya shughuli mbalimbali katika ukanda huu wa pembezoni mwa Bwawa watusaidie kuhakikisha kwamba wnakuwa nje ya Mita 60 lakini wajitahidi kuitunza miti hii ambayo ipo katika mashamba yao” Amesema Eng. Tamim.

Katika hatua nyengine, Eng. Tamim, amesema MORUWASA imetenga kiasi cha fedha chenye thamani ya shilingi Bilioni 185 kwa ajili ya maboresho ya huduma za maji Manispaa ya Morogoro ikiwamo kupanua Bwawa la Mindu pamoja na kununua mtambo mpya.



 

 

 

 

 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.