MBUNGE ABOOD , AWATAKA UWT MOROGORO MJINI KUBUNI NA KUANZISHA MIRADI ENDELEVU YA KUSAIDIA JAMII.
UMOJA wa Wanawake Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi CCM , Manispaa ya Morogoro wametakiwa kubuni miradi ya kimaendeleo kwa
lengo la kupunguza kuomba misaada na kubwa zaidi kujiimarisha kwenye uchumi ili
kuunga mkono kauli mbiu ya Uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, leo Desemba 30/2020 katika
Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Matawi na Kata wa UWT CCM Wilaya ya Morogoro Mjini katika
Ukumbi wa Mango Garden Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari,
Mhe. Abood, ameitaka UW T Wilaya ya Morogoro Mjini, kubuni miradi na kuendeleza
miradi waliyonayo kama jumuiya nyingine zinavyo fanya na kuwataka kuwa na
miradi yao binafsi ili kupunguza tabia ya kutembea na mabakuli kuomba.
Mhe. Abood, amesema kuwa ,CCM imekuwa ni taasisi bora ya kisiasa inayotekeleza miradi endelevu inayogusa maisha ya wananchi wa ngazi zote katika jamii.
“Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kuaminiwa na
Wananchi wa Morogoro Mjini kama nguzo na kimbilio la kupata Majawabu ya uhakika
kwa matatizo yanayowakabili, hivyo niwaombe Viongozi wa Jumuiya hii mshikamane
, uchaguzi umekwisha, mimi Mbunge wenu kwa kushirikiana na Chama nitahakikisha
Jumuiya hizi zinakuwa na shughuli za kufanya kwa kubuni miradi mbalimbali,
jukumu letu sisi viongozi ni kuhakikisha
tunawasaidia kuwawezesha ili kuanzisha vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha
viwanda ambavyo vitatoa ajira "Amesema Mhe. Abood.
Katika hatua
nyengine, Mhe. Abood, ameahdi kutoa fedha katika Jumuiya hiyo ili wabuni mradi
mbalimbali itakayoweza Jumuiya hiyo
kusimama yenyewe katika kukabiliana na mfumo tegemezi na kuweza kujikwamua na umasikini.
Mwisho, Mhe. Abood, amesema uchaguzi umeisha kilichobakia ni
Viongozi kuweka nguvu moja katika kuwatumikia Wananchi na kufanya vile walivyoahidi
ili kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025.
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Sofia Kibaba,
amewataka Viongozi walioshinda wtekeleze kikamilifu ahadi zao ili kuwaletea
wananchi maendeleo.
Kibaba, amesema kilichobakia sasa baada ya uchaguzi ni
kuhakikisha Jumuiya zinajengwa na kuongezewa nguvu ili zizidi kuimarika.
“ Kama alivyosema Mbunge wetu suala la miradi haliepukiki,
lengo la miradi kusaidia kazi za Chama zifanyike kwa ufanisi zaidi kuliko
kutegemea mifuko ya watu , kama tusipokuwa na miradi hatutokuwa wakali na
tutaendelea kubakia dhaifu lakini kama tuna miradi tutakuwa wakali hata katika
kusimamia maamuzi yetu na kusongesha chama mbele “ Amesema Kibaba.
Hata hivyo, Kibaba, amesema kutokana na agizo lililotoka
ngazi za juu, amewataka Viongozi wote ambao wanavyeo viwili baada ya uchaguzi kwa
mujibu wa agizo wanatakiwa kuoandika barua ya kujiuzuru cheo kimoja ili
waachie watu wengine waendelee kushika nyadhifa hizona zoezi la uchaguzi
lilatolewa taarifa ili watu waanze kuchukua fomu.
Pia amewataka wale wote waliokosa nafasi katika kinyang’anyiro
cha uchaguzi wa ndani ya Chama , wasikate tama kwani chama kina nafasi nyingiza
kufanya kazi.
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro
Mjini, Bi. Victoria Saduka, amesema wao wamejipanga kufanya siasa za
uchumi na si siasa za maneno .
Saduka,
amesema kuwa katika kuona hilo linafanikiwa atahakikisha kupitia Viongozi wa
Jumuiya hiyo wataanzisha miradi pamoja na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa Jumuiya hiyo ya UWT ili wajiajiri katika
masuala ya ujasiriamali.
Amemuomba
Mhe. Abood, kuendelea kuwashika mikono Wakina mama kwani wao walikuwa katika
mstari wa mbele kuhakikisha Chama Cha
Mapinduzi kinaendelea kushika dola hususani katika kuhakikisha Mhe. Abood
anarudi madarakani.
“Mhe.
Abood, katika watu waliojitoa kuhakikisha unarudi madarakani, UWT hawa wakina
mama wamefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha unapita kwa kishindo, asilimia
kubwa ya kula zimetokana na wakina mama, tunakuomba usituache tushike mkono
kwani wakina mama hawa wana imani kubwa sana na wewe hivyo tunaamini uwezo unao
utawasaidia ili kufikia malengo” Amesema Mama Saduka.
Naye
Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Rehema Malindi, amewataka Wanawake kuwa
mfano bora wa kufanya kazi kwa kujiamini ili kujikwamua kiuchumi.
Malindi, amesema kuwa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, wamekuwa
katika mstari wa mbele katika kujitokeza
kwa wingi katika masuala mbali mbali ya kuimarisha CCM na Jumuiya zake.
“ Leo tumeitana hapa lakini lengo kubwa ni kumpongeza Mhe.
Abood , kwa kupata kura za kishindo na kufanya Jimbo letu kuongoza Kitaifa kwa
kura nyingi za Mhe. Rais, hii inatupa faraja kwamba Morogoro tumekuwa kioo kwa
Taifa, uchaguzi umekwisha nguvu zetu tuzielekeze katika kujenga Jumuiya zetu,
tunaye Mbunge makini tumtumie vizuri ili tujenge fursa mbalimbali katika
Jumuiya “ Amesema Malindi.
Shughuli hiyo ilienda sambamaba na Mkutano wa Baraza la UWT Wilaya ya Morogoro Mjini huku ikishuhudiwa tukio la Viongozi kupewa vyeti vya shukrani kutokana na kujitoa kwao katika kazi mbalimbali ndani na nje ya CCM .
Post a Comment