Header Ads

Ukishindwa Kuendana Na Kitu Hiki, Sio Rahisi Kwako Kuweza Kufanikiwa

Kushindwa kwenye maisha wakati mwingine kunakuja si kwa sababu huna malengo au huchukui hatua, bali kuna wakati unashindwa kwa sababu ya kushindwa kuendana na mazingira yanayokuzunguka.

Kuna wakati naweza nikasema unaweza ukashindwa kuendana na mazingira ya aina tofauti tofauti kama vile  mazingira ya ushindani katika biashara na mazingira mengineyo ambayo yanakupa upinzani sana.

Kwa vyovyote vile ili uweze kujihakikishia ushindi wa mafanikio, unatakiwa uwe ni mtu wa kuendana na mazingira yanayokuzunguka yaani uwe na ule  uwezo  wa ‘ku- adapt.’ Hali yoyote unapokutana nayo ni lazima kwako ujue jinsi ya kuishinda.

Vitu vyote vinavyoshindwa kuendana na mazingira mara nyingi huwa vinashindwa sana au hata kuweza kufa kabisa. Hili unaweza ukaliona kwa wanyama na hata mimea  pia. Viumbe hivyo hujitahidi sana kuendana na mazingira halisi.

Hata wewe unapokutana na tukio au hali yoyote hata kama hali hiyo inaonekana ni ngumu sana kwako lakini unatakiwa kujua jinsi ya kukabilina nayo hali hiyo. Ukishindwa kukabiliana na hali hio utashindwwa tu huko mbeleni.

Kuelewa vizuri hili, hebu angalia mimea ambayo inakua jangwani ni kitu gani ambacho hutokea? Ni kwamba mimea hiyo huweza kumudu kuweza kuishi kwenye mazingira kwa kuweka mizizi mirefu au kuwa na miiba sana.

Inabidi na wewe ujue, unapokutana na kipindi kigumu kwenye maisha yako ujue namna ya kuweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuishinda. Kama utakuwa ni mtu wa kulia, nakuhakikishia utaweza kushindwa kwa kila kitu.

Badilika kulingana na mazingira unayokutana nayo. Usikubali kila wakati kuwa mtu yule yule ambaye huna uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira unayokutana nayo. Kama unapitia kipindi kigumu cha maisha komaa kweli hadi ushinde.

Nakukahakikishia utakuwa mshindi katika maisha kama kila wakati wewe utakuwa ni mtu ambaye unaweza kubadilika kulingana na mazingira yako au kuwa na ule uwezo wa kuendana kulingana na hali halisi.

Kama hunielewi vizuri yaani hapa, namaanisha unatakiwa uwe na uwezo wa kuishi popote na kufanya chochote kama inatokea mazingira uliyopo yanakulazimisha wewe kuweza kufanya hivyo, hiyo itakuwa na msaada mkubwa sana kwako.

Usilie au kuhuzunika kwa sababu uchumi ni mbovu au unaona mambo siku hizi yamekuwa tofauti na zamani. Unatakiwa kukazana na kuweka juhudi sana hadi kuweza kufanikiwa. Hiyo yote itafaa kama utaendana na hali inayokuzunguka.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.