UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
UMOJA wa Wanawake wa Tanzania, Wilaya ya Morogoro Mjini (UWT) ,wameadhimisha siku ya wanawake duniani ikiwa na lengo la kujadili masuala ya ustawi wa Jamii na kufurahi kwa pamoja kutokana na mafanikio wanayoyapata.
Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 08/2024 kwenye Ukumbi wa Mango Garden huku mgeni rasmi akiwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Christine Ishengoma.
Dkt. Ishengoma, amewasisitiza wanawake wa Mkoa wa Morogoro kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono na kumlinda Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Dkt. Ishengoma, amesisitiza Viongozi wa UWT Mkoa wa Morogoro na mikoa mingine kwa ujumla kubeba Ajenda za Maendeleo ya Wanawake na Watoto na kupambana kutatua changamoto zao maana ukimuinua Mwanamke umeiinua Jamii nzima.
'Kama kawaida Jambo Letu la 2025 ✅ #UWTImara #JeshiLaMama,tuoneshe Ujeshi wetu, tumsemee mama na kumuhakikishia ushindi wa kishindo 2025, lakini hili litawezekana kama 2024 tutasimama na wenyeviti wetu wote wa Mitaa kupata ushindi wa kishindo" Amesema Dkt. Ishengoma.
Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Morogoro, Bi. Mwajabu Maguluko, amewataka UWT Mkoa wa Morogoro kuwa na umoja ili kutimiza majukumu yao ya kiutendaji na kuhakikisha UWT inazidi kuwa imara.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Victoria Saduka, amepongeza kamati ya maandalizi pamoja na Wabunge Viti Maalum, Wenyeviti na Makatibu , Madiwani Viti Maalum kwa kufanikisha maandalizi ya maadhimisho hayo.
Saduka, amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za Uongozi Serikali za Mitaa 2024 ili kuongeza wigo wa wanawake katika ngazi za Uongozi .
Mwisho, Saduka, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuwatengenezea mazingira rafiki wanawake na kuwaamini katika nafasi za Uongozi kupitia teuzi anazozifanya.
Post a Comment