Header Ads

JUMUIYA YA AHMADIYYA MOROGORO YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA ZAIDI YA KAYA 160 ZENYE UHITAJI.



JUMUIYA ya Kiislamu ya Ahmadiyya Morogoro imetoa msaada wa vyakula kwa zaidi ya  Kaya 160 zenye uhitaji kutoka Mitaa ya Ngerengere, Kitata, Msamvu B, Mtaa wa Mbuyuni pamoja na Mtaa wa Airport iliyopo  Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro ikiwa ni chakula ikiwa ni sadaka katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambapo utaratibu huu wamekuwa wakiufanya kila mwaka.

Hafla hiyo fupi ya ugawaji wa vyakula imefanyika Machi 23/2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ahmadya Kihonda Maghorofani.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ugawaji wa vyakula,Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebecca Nsemwa,  ambaye ndiye mgeni katika hafla hiyo, ameushukuru Uongozi wa Ahmadyya, kwa kujitoa kwao hususani katika kutoa huduma ya elimu kwa kuwa na shule zao, huduma ya afya katika Hospitali zao pamoja na kutoa huduma ya kiroho.

"Wenzetu Ahmadyya licha ya kugawa zawadi hii katika kuwajali ndugu zetu kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lakini wanatukumbusha kuwa na upendo pamoja na kusaidiana, hili sio jambo dogo , ni jambo la kiimani lenye kumpendeza Mwenyezi Mungu, ukiwa na roho ya uchamungu hata mambo yako yanafanikiwa, tumeona rushwa, uongo , dhuruma, ufisadi , ulawiti haya yote ni matokeo ya kutokuwa mchamungu na kukosa hofu ya Mungu" Amesema DC Nsemwa.

DC Nsemwa ,  amewataka wazazi kuhakikisha watoto wanawalea katika maadili ya kumcha Mungu ili kuweza kuwa na Viongozi watakaoongoza Tanzania katika imani na misingi ya Kimungu.

Aidha, DC Nsemwa,  amewataka Wazazi kujitoa  katika kujifunza jinsi ya kuwalea watoto katika misingi halisi ya kumjua Mungu.

Kwa upande wa Amiri na Mabshiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, amesema  kuwa dini ya kiislamu ni dini ya amani na upendo na dini yenye mafundisho ya kujaaliana kama wanajamii.

Aliweze kuelezamsimamo wa jumuiya ya Ahamdiyya kwamba ni jumuiya inayohubiri amani na upenda kwa wote bila chuki kwa yeyote na inahubiri huheshimu dini zote na kuishi katika mazingira ya kuhurimiana .

Sheikh Chaudhry, amesema  kwamba Jumuiya ya Ahamdiyya , kama Jumuiya haishiriki katika  siasa ya nchi , na inayo sera  ya kutii Serikali  iliyoko madarakani na kushirikiana na Serikali katika  kujenga Jamii yenye maelewano na Jamii yenye maendeleo.

Pia , Sheikh Chaudhry, amefundisha kwamba  sawa na mafundisho ya Mtume Mtukufu wa Kiislam kuipenda nchi na kuitakia maendeleo na kulitumikia Taifa ni sehemu ya imani ya Mwislamu.

Naye Mkuu wa Chuo cha Jumuiya ya Ahmadiyya Morogoro, Sheikh Abid Mahmood Bhatti, amesema kuwa  msaada huo umetolewa kuunga mkono wito wa serikali inayohimiza mashirika,taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.

Bhatti, amesema licha ya kuunga mkono Serikali  lakini pia kuweza kutoa zakatul Fitri kwa jamii ili kuweza kujumuika na jamii katika kusherehekea Sikuu ya Eid Fitr.

"Jumuiya ya Ahmadiyya ni moja ya sehemu inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo ya kiafya,kielimu na kijamii kwa kuwafikia watu wenye uhitaji, hivyo kutoa kwetu chakula kwa watu wenye uhitaji kwanza tumetekeleza misingi ya dini , kwani sisi tumekuwa tukifanya hivi kila ifikapo Siku ya Eid basi tumekuwa tukijumuika na ndugu zetu kuhakikisha kwamba tunakuwa nao pamoja katika kusheherekea sikukuu hii " Amesema Bhatti.

Miongoni wa vyakula hivyo vilivyo gharimi takribani Shilingi Milioni 3 na zaidi, ni  pamoja na Mchele mfuko wenye  Kilo 5 na Unga wa Sembe Mfuko wa Kilo 10.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.