Header Ads

DIWANI BUTABILE ATETA NA VIONGOZI WA CHAMA NA MABALOZI WA MASHINA KUELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE


DIWANI wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile,  amewapongeza Mabalozi wa mashina ya CCM  kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda na kukipigania Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ameitoa Wakati wa kikao kazi cha Mabalozi hao kilichofanyika Ofisi ya CCM ya Kata ya Mafiga Machi 29/2024.

Akizungumza na Mabalozi hao, Mhe. Butabile, amesema  Mabalozi  wa Mashina ndio wanaobeba na kusimamia ajenda ya Chama Cha Mapinduzi, huku akisema yeye kwa kushirikiana na Uongozi wa CCM wa Kata  na BMK ya Kata hawatawaangusha  katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

"Tunapojiandaa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa 2024  hatuna mashaka kwa sababu Viongozi wa mashina wameshaamua Kata hii ya Mafiga iendelee kutawaliwa na CCM pamoja na Jimbo la Morogoro Mjini , sisi kama Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wetu wa CCM wa Kata na Matawi tutaendelea kuwaunga mkono ili kuleta ustawi wa Chama Chetu na kuhakikisha chaguzi zote tukianza na wa Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025  tunashinda kwa kishindo" Amesema Butabile.

Aidha, Mhe. Butabile , amempongeza  na  kumshukuru Dkt, Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa za ujenzi wa miradi ya Maendeleo  Kata ya Mafiga hususani katika sekta ya Afya, Elimu na huduma za Jamii kama vile TASAF na mfuko wa uwezeshaji kupitia mkopo wa asilimia 10.

Mwenyekiti wa Chama wa Taifa ambaye pia ni Rais wetu wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan anawajali nasi hatuna budi kuwajali na kuwaheshimu Mabalozi wa  Mashina, tunakila  sababu ya kujivunia mambo mazuri yaliyofanywa na serikali, ili kuimarisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi tunahitaji kupendana na kusemea mazuri, kama Chama tuna utaratibu wetu wa kukosoana hivyo haipendezi viongozi wa Chama tukawa tunatupiana  vijembe katika hadhara ya watu ,lakini tuendelee kuombeana yote haya nayafanya kwa ajili ya kulinda Chama Chetu Cha Mpinduzi CCM " Ameongeza Butabile.

Hata hivyo, Butabile, amesema kuwa  Mabalozi ni watu muhimu kwa uhai na utendaji wa kazi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndio wanaopokea kero za wananchi.

Butabile, amewataka Mabalozi na wananchi wa Mafiga kuendelea  kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi, kumuamini  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , pamoja na Viongozi wa Serikali za Mitaa na watumishi waliopo katika Kata hiyo.

Mwisho, Butabile, amesema  katika kujenga Chama Mabalozi wahamasishe wanachama katika kulipa Ada ya chama na kufanya mikutano na wananchi kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

"Niwaombe Mabalozi muendele kufanya kazi ya kusajili wanachama wapya Ile wale wasio wanachama wawe wanachama wa Chama Cha Mapinduzi," Amesisitiza Mhe. Butabile.

Kwa upande wake, Katibu wa Tawi la CCM Misufini, Ndg. Esther Lyombile, amemshukuru Mhe. Diwani  kwa kuwathamini na kukaa pamoja na  Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya Shina ikiwa na lengo la kuimarisha uhai wa Chama na Jumuiya zake.

Miongoni mwa Mabalozi wa Mashina , Ndg. Sudi Kiswanya, Balozi Shina No.6 Tawi la Tanki la Zamani, amempongeza Mhe. Butabile kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuiletea Mafiga Maendeleo hususani katika miradi ya afya, elimu na kuleta chachu ya maendeleo kwa Kata hiyo.

Mhe. Butabile, ameanza mikutano ya kuzungumza na Viongozi wa Chama ikiwemo Wenyeviti wa Chama wa Matawi, Makatibu, Wenezi na sasa Mabalozi wa Mashina na anatarajia kukutana na Viongozi wa Jumuiya zote za Chama ikiwa na lengo la kuimarisha uhai wa  Chama na Jumuiya pamoja na kuzungumza juu ya utekelezaji wa Ilani katika kipindi chake cha miaka 3 ya Uongozi wake.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.