Header Ads

KILAKALA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, VIONGOZI WATEMA CHECHE

KATA ya Kilakala Manispaa ya Morogoro  wameadhimisha sherehe ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani likiwa zimebaki siku chache kwa maadhimisho hayo kufika kileleni.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 06/2024 katika Ukumbi wa Chilakale kwa kushirikisha wajasiriamali  na vikundi mbalimbali vya wanawake.

Akizungumza na wanawake hao, Diwani wa Viti Maalum ambaye ndiye mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, Mhe. Mwanaidi Ngurungu, amewataka wanawake kuwa vipaumbele katika kutetea watoto wakike na wakiume kwa kuwapeleka shuleni pamoja na kusimamia mienendo yao ya kitabia.

" Niseme tu kwamba  sisi wanawake ndo wasemaji wa watoto wetu wewe mama ukinyamaza kusema hakuna atakaye mkomboa mwanao wanawake tuwapeleke watoto wetu shule anayestahili kuanza chekechea aanze pia kidato cha kwanza aanze kwa maana hao ndo Madaktari wa kesho msikatishe ndoto za watoto wapeni haki ya kusoma lakini pia uwe namba moja kufuatilia tabia za mtoto wako shuleni pamoja na nyumbani tusiwaachie waalimu peke yao" Amesema Ngurungu.

Aidha, Mhe. Ngurungu, ametoa rai kwa mwanamke achukue jukumu la lakuwa karibu na watoto kujua marafiki zake , kutambua aina ya michezo anayocheza mtoto akiwa na wenzake, na kutambua maendeleo yake ya shule .

Naye, Diwani Viti Maalum mbaye pia ni mlezi wa Kata hiyo,  Mhe. Grace Mkumbae, akiwa katika sherehe hiyo amesema wanawake wamekuwabize nashughuli kuliko kufatilia maendeleo ya watoto kuanzia maisha ya nyumbani mpaka shuleni hali inayopelekea watoto wengi kuharibikiwa wakiwa na umri mdogo bila hata wazazi kujua.

" watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa aina nyingi ikiwemo kubakwa na kulawitiwa kutokana na wazazi kutokuwa makini na watoto , tuchukue nafasi zetu wakina mama kutimiza wajibu katika malezi ya watoto wetu" Amesema Mhe. Mkumbae.

Aidha, Mkumbae,  amewataka wanawake kukaa na watoto wao wakike  kuongea nao kuwaeleza hali halisi ya maisha pasipo kuwaficha ili kuweza kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kilakala, Juliana Mwenda, amewataka wanawake kushikamana na kutumie fursa za vikundi ili kuepuka mikopo isiyo na tija (kausha damu).

Akitoa salamu za Kata, Diwani wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga, mewataka wazazi na walezi Kata ya Kilakala  kuwalea watoto wao katika maadili mazuri yenye kulinda mila na desturi ili kuendeleza utamaduni wa kitanzania.

Kanga, amesema wazazi na walezi wanawajibu mkubwa wa kuwafundisha watoto wao maadili yanayofuata misingi ya Nchi ili kuthibiti wimbi la mmomonyoko wa maadili katika kizazi hiki.

Aidha, amesema kuwekeza kwenye uhifadhi wa tamaduni, mila na desturi za asili inasaidia kuimarisha utulivu na amani ya Nchi ikiwa ni pamoja na kuzuia migogoro mbalimbali kwenye jamii.

"Niwaombe sana wazazi tuwekeze kwenye malezi na makuzi ya mtoto yanayohifadhi utamaduni wa asili ili kulinda mila na desturi za kitanzania, kufanya hivyo itasaidia watoto kukua katika maadili mema yanayozingatia utamaduni, mila na desturi za makabila yao katika mavazi, heshima na mambo mengine muhimu, na katika vikao wenyeviti ukatili wa kijisnia iwe agenda yenu "Amesema Mhe. Kanga.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.