KAMATI YA HUDUMA MAFIGA YAKOSHWA NA UTENDAJI KAZI VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
KAMATI ya Huduma za Jamii Kata ya Mafiga imeridhishwa na utoaji wa huduma ya afya kwa Vituo vya kutolea huduma vilivyopo kwenye Kata hiyo.
Kauli hiyo imesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mafiga , Mhe. Thomas Butabile Machi 14/2024 ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za Watumishi.
Butabile, amesema Kamati hiyo imekuwa ikitembelea miradi mbalimbali lakini ziara ya Machi 14/2024 imelenga haswa kutembelea maeneo ya kutolea huduma za afya kwa Vituo vya Serikali na vya watu binafsi.
" Kamati imefarijika sana, huduma ni bora na wananchi wetu wanaridhika na huduma zao, changamoto tumezibeba tunakwenda kuzifanyia kazi na sehemu ambayo inahitaji maelekezo tutatoa maelekezo kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za afya" Amesema Butabile.
"Kata yetu ina jumla ya Vituo 6 vya huduma ya afya ukichukua hiki Kituo kikubwa cha mafiga na vituo vya watu binafsi nina maanisha Zahanati na Maabara, niendelee kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kutoa huduma kwa wananchi wetu, sisi sote tunaihudumia jamii kwahyo hatunabudi kufahamiana na kuleta mahusiano ndani ya kata yetu hivyo tunapaswa Kushirikiana, na kama kuna changamoto zozote tuambizane ili tuweze kuzitatua"Ameongeza Butabile.
Aidha, amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuleta mahusiano baina ya Taasisi za Umma na za watu binasfi ili kuleta ufanisi na maendeleo chanya katika Kata ya Mafiga.
Kwa upande wa watumishi wa baadhi wa vituo vya afya wa meeleza kero yao kubwa Ni barabara kwa kuwa inaweza kupelekea maumivu makali kwa mjamzito au mtu yeyote aliyefanyiwa upasuaji kwa kuwa barabara hizo zina mashimo hivyo wameomba zifanyiwe ukarabari ili kuepuka adha hiyo.
Pia, wamefafanua kero nyingine Ni uzoaji wa taka kwa kuwa taka zinakaa muda mrefu bila kuzolewa kitu ambacho siyo rafiki kwa afya zetu.
Mwisho watumishi na watoa huduma wa vituo wamempongeza Mh Butabile na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuonesha ushirikiano kuja kufanya ziara katika vituo vyao na kuwataka waendelee na ziara za aina hiyo kwa kuwa wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Post a Comment