Header Ads

ADRA KWA KUSHIRIKIANA NA TAS WAFUNGUA MFUKO WEZESHI WA ELIMU KWA WATU WENYE UALBINO

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Adra Tanzania,( Adventist  Development and Relief Agency (ADRA) kwa kushirikiana na Chama  Cha Watu wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro (TAS) wamezindua mpango maalumu wa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha mfuko wa uwezeshaji wa elimu kwa wafunzi wenye Ualbino Mkoa wa Morogoro.

Harambee hiyo ya uchangiaji imefanyika katikaUkumbi wa Soko Kuu la Chifu Kingalu Machi 27/2024 kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo ya uchangiaji wa mfuko wa wanafunzi wenye Ualbino,  Afisa Ustawi Ofisi ya Manispaa ya Morogoro  ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya TAS , Rehema Malimi, amesema kuwa ADRA limekuwa ni miongoni mwa mashirika ambayo ni mkombozi kwa watu wenye ualbino nchini kwani wamekuwa na programu mbalimbali na miradi ambayo imekuwa na manufaa kwa watu wenye ualbino hususani Mkoa wa Morogoro.

" Nawapongeza ADRA kwa kushirikiana na TAS kwa kuja na mradi huu , kwani watu wenye Ualbino wamekuwa wakipitia katika changamoto nyingi sana za kimasiha hususani wanafunzi ,unakuta wazazi hawana fedha za kuwasomesha wanarudi nyumbani na kukatisha ndoto zao, kuja kwa mfuko huu utasaidia sana kuhakikisha unaleta matokeo chanya na kutatua changamoto zinazo mkabili mtoto mwenye Ualbino husuani katika mahitaji yake ya shule" Amesema Malimi.

Naye Mratibu wa Makundi ya watu wenye Ualbino Manispaa ya Morogoro, Devid Max, amesema makundi ya watu wenye Ualbino ni makundi ambayo yanahitaji msaada mkubwa kwani mfuko huo utaenda kupunguza changamoto za mwanafunzi mwenye Ualbino kwa kupata mahitaji muhimu ya elimu nakumfanya kutimiza  ndoto zake.

Mratibu wa ADRA Mkoa wa Morogoro , Marry Yonaz,  amesema mfuko huu wezeshi wa elimu utakuwa ni msaada sana kwa watoto wenye ualbino kwani zile changamoto ambazo zinawakumba watoto wenye  ualbino za gharama za mahitaji ya shule watakuwa wameenda kutibu kidonda cha wazazi ambao wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za elimu kama vile mavazi, madaftari n.k.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.