MJUMBE KAMATI UTEKELEZAJI UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI AGAWA KADI ZA BIMA YA AFYA CHF KWA WAZEE 51 KATA YA LUHUNGO
JUMLA ya kaya 30 za wazee Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro zimepatiwa msaada wa bima za afya ICHF zilizoboreshwa kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Morogoro Mjini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee.
Kadi hizo zimetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Josephine Kapoma Machi 27/2024 kwenye Ofisi ya Kata ya Luhungo.
Akizungumza na Wazee waliojitokeza kwenye ugawaji huo wa Bima , Kapoma, amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuwekeza kwenye afya za wazee kwani ni kundi muhimu katika jamii ambalo linapaswa kupawa kipaumbele kwenye huduma za kijamii.
Kapoma, amewataka Wazee hao kutunza kadi hizo zitazowawezesha kupata huduma za afya bure bila kulipia .
Diwani wa Kata ya Luhungo, Mhe. Abdallah Chamgulu,amemshukuru Bi. Josephine kwa kuwaangalia kwa jicho la huruma na hakika wanaona wapo watu wanao wajali na kuwathamini.
“Tunamshukuru Dada Josephine kwa kuwajali wazee wetu wa Luhungo, faida ya bima hizi za afya zinamfanya mzee huyu kupata huduma zote za afya bure na bila ya kuwa na ule usumbufu wa kwenda kwa Mtandaji wa Kata na Mtendaji wa Mtaa ili aandikiwe barua” Amesema Chamgulu.
Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Luhungo,ambaye pia ni Diwani Mstaafu wa Kata ya Luhungo, Rajabu Mizambwa,amemshukuru Bi. Josephine, kwa kuwajali na kuwathamini kwani wazee hao walikua na changamoto ya matibabu kutokana na uwezo mdogo wa kifedha hivyo watapata fursa ya kutibiwa .
Post a Comment