MBUNGE ABOOD AJITOSA KUKABILI ADHA YA MAJI YA MVUA YANAYO WAATHIRI WANANCHI WA MBUYUNI , ACHANGIA MILIONI 1 NA KUENDESHA HARAMBEE KWA WANANCHI
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mh. Dkt. Abdulaaziz Abood, amechangia shilingi Milioni moja kwa ajili ya kurahisha utoaji wa maji ya mvua ambayo yamekuwa yakiwaathiri wananchi wa Mtaa wa Mbuyuni Kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro.
Hayo ameyafanya Machi 21/2024 katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa Kata hiyo katika Mitaa ya Mbuyuni, Kayenzi na Kilimahewa.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara, Mhe. Abood ,amesema wananchi wamekuwa wakiishi katika hali ya kukosa matumaini wakati wa mvua hivyo lazima maji hayo yanayo waathiri yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Aidha, Mhe. Abood ameendesha harambee ya kuchangia fedha hizo za kuaondoa maji hayo ya mvua ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi laki 507,000/= zilichangishwa huku Diwani wa Kata hiyo akitoa shilingi 200000/= kama sehemu ya mchango wake.
Katika michango hiyo baadhi ya wananchi mmojammoja pamoja na makundi ya watu walijitokeza kuchangia huduma hiyo kutokana na kukerwa kuwepo kwa maji hayo ambayo yamekuwa ni adha kubwa kwa wananchi wa Mbuyuni.
Katika upande wa Elimu, Mhe. Abood, amesema Serikali inajenga miundombinu,inaleta walimu hivyo ni wajibu wa wazazi kuwaandaa watoto ikiwa ni pamoja na kuwanunulia sare za shule na chakula ili waweze kuzingatia masomo yao darasani na kufaulu vizuri.
Pia, amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwafundisha maadili mema kwani kuna wimbi la mmong'onyoko wa maadili jambo ambalo sio utamaduni wa Mtanzania.
Naye Mhandisi ujenzi miradi ya maji MORUWASA , Eng. Stephen Tungu, amesema hadi huduma hiyo ya maji ya mvua yanayo waathiri wananchi wa Mtaa wa Mbuyuni kuondolewa , kiasi cha shilingi 2,725,000/= kinahitajika katika kufanya kazi hiyo.
"Nimepokea hundi yenye thamani ya milioni 1000000/= kutoka kwa Mhe. Abood, na kama maelekezo alivyoyatoa ni kwamba fedha zote za michango zitapitia kwetu hadi pale fedha zikikamilika ambapo jukumu letu litakuwa ni kuhakikisha maji hayo tunayaondoa na wananchi wanakuwa katika mazingira rafiki wakati wa mvua kunyesha " Amesema Eng. Tungu.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mafisa, Mhe. Joel Kisome, amempongeza Mh. Abood kwa kujitoa kwake katika kuchangia miradi ya maendeleo katika Jimbo la Morogoro Mjini.
“Tunatambua kazi kubwa unayoifanya katika Jimbo letu la Morogoro hususani katika Kata yetu ya Mafisa, unaomba utufikishie salamu zetu za shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya,kila tukitembea tunaona maendeleo aliyoyafanya kwa ajili yetu,tunshukuru sana,”Amesema Mhe. Kisome.
Kuhusu miundombinu ya barabara, Mhe. Kisome, amesema wana mpango mkubwa wa kufanya ukarabati wa barabara zao mara baada ya hali ya hewa kuimarika na kukata kwa mvua.
Mhe. Abood, anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero za wananchi, ambapo ziara hiyo itaendelea Machi 22/2024 katika Kata ya Mzinga ambapo atatembelea Shule ya Sekondari Konga na Zahanati ya Konga na kufanya mkutano wa hadhara na upande wa Kata ya Kauzeni atatembelea Zahanati ya Kata ya Kauzeni, Choo cha Shule ya Msingi Kauzeni , maabara ya Sekondari kauzeni pamoja na kufanya mkutano wa hadhara.
Post a Comment