GREEN APPLE SCHOOL YAPAA KIMATAIFA, YATUNIKIWA MEDALI ZA KIMATAIFA NCHINI INDIA
WANAFUNZI wa Shule ya Green Apple Pre & Primary wametunukiwa Medali za Kimataifa baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya sanaa yaliyoandaliwa na Shirika la Rangotsav Celebration nchini India.
Medali hizo wametunikiwa Machi 06/2024 katika hafla fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Green Apple kwa ajili ya kuwatia moyo na kula chakula cha pamoja kwa kazi nzuri waliyofanya wanafunzi wao kwa kuwakilisha nchi katika michezo ya sanaa.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa medali hizo ambazo zilishatunikiwa na wanafunzi wakiwa nchini India, Afisa Michezo Mkoa wa Morogoro , ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi hao , Riziki Mguhi, amewapongeza wanafunzi wa Green Apple kwa kuwakilisha Nchin vizuri na kuiletea heshima Shule yao , Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Riziki, amesema amehimiza michezo iendelee kuboreshwa kwani michezo humjenga mtoto kimwili na kiakili.
Aidha, ameuomba Uongozi wa Green Apple kuboresha eneo lamichezokKwa kuzingatia umri wa watoto watoto ili hata wale wa umri mdogo wapate muda wa kushiiri ktk michezo mengine mbalimbali
Hata hivyo,amehimiza shule zote za Mkoa wa Morogoro ikiwemo Green Apple kuhimiza wanafunzi wao kushiriki mashindano ya UMISHUMTA na michezo mbalimbali isiyotumia gharama kama vile kukimbia, kurusha tufe, kuvuta kwamba nk.
Pia , amechukua nafasi hiyo kupongeza uongozi wa shule , walimu pamoja na wanafunzi kwa kuweza kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa na kuahidi kushirikiana na shule kuhakikisha michezo inapewa kipaumbele Kwa ajili ya ustawi wa mtoto.
Naye Mkurugenzi wa Shule ya Green Apple, Mwajabu Dhahabu, amesema michezo hiyo amabyo shule yake ilishiri, ilishirikisha shule mmbalimbali za Msingi Duniani ambapo shule ya Green nayo ilipata bahati ya kushirikia ktik mashindano hayo.
Dhahabu, amesema katika michezo hiyo, jumla ya wanafunzi 120 walishiriki mashindano hayo ya sanaa na kati ya watoto hao ni wanafunzi 19 walifanya vizuri na kutunukiwa medali za Kimataifa (International Medal) pamoja na kombe (Merit award).
Mara baada ya kutangazwa washindi na walioshinda kutunukiwa medali za Kimaitafa wanafunzi wote ambao walishiriki walizawadiwa vyeti vya ushiriki katika michezo hiyo ya sanaa.
Miongoni mwa michezo ambayo ilishindaniwa ni michezo ya sanaa ya uchoraji, upakaji rangi, upigaji picha pamoja na shindano la muandiko.
"Wanafunzi wangu walipata mwaliko wa michezo ya sanaa nchini india, nawashukuru sana wanafunzi wangu kwa kututoa kimasomaso pamoja na wanafunzi wote walioshiriki lakini nichukue nafasi hii kuwapongeza waalimu wangu kwa kazi nzuri ya kuwajengea uwezo wanafunzi katika stadi za maisha na hatimaye kurudi na medali za Kimataifa " Amesema Dhahabu.
Post a Comment