KAMATI YA HUDUMA KATA YA MAFIGA YAFANYA ZIARA YA KAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI.
KAMATI ya Huduma Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro chini ya Diwani wa Kata hiyo Mh Thomas Butabile imeanza ziara Machi13,2024 ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto katika sekta mbalimbali.v
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Butabile, amsesema lengo la ziara hiyo ni kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inatoa huduma kwa wananchi pamoja na kusikiliza kero za watumishi ili kuona namna ya kuzitatua.
Kamati hiyo, imefanya ziara hiyo katika sekta ya elimu kwa kutembelea shule zote zilizopo katika kata hiyo.
Aidha, Mhe. Butabile, amesema katika shule za Kata ya Mafiga maendeleo ya kitaaluma yanazidi kuimarika siku hadi siku jambo ambalo linawafariji licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Hata hivyo, Mhe. Butabile, amesema bado kuna changamoto ya wastani wa vyoo vya wanafunzi kwa upande wa wasichana na wavulana licha ya kuanza kuchukua jitihada binafsi ambapo katika shule ya msingi Misufini B tayari ujenzi wa matundu ya vyoo 10 yameshakamilika na wanasubiria kukabidhiwa na mafundi kwa ajili ya wanafunzi kuanza kuvitumia.
Pia, licha ya uhaba wa matundu ya vyoo lakini changamoto nyengine ambayo inazikumba shule za Kta hiyo ni uhaba wa madawati , upunguvu wa vyoo, viti na meza vya wanafunzi, na baadhi ya shule za msingi kutokuwa na waalimu wa kutosha.
Mwisho, Mhe. Butabile kwa niaba ya Kamati hiyo ,amesema changamoto zote ambazo wamekutana nazo wataenda kuzifanyia kazi ili kuharakisha haraka maendeleo ya Kata hiyo.
Ziara hiyo ni ya siku mbili ambayo imeanza Machi 13/2024 na inatarajia kumalizika Machi 14/2024
Post a Comment