Header Ads

MKOA WA MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


MKOA wa Morogoro waadhimisha siku ya Wanawake Duniani  , huku maelefu ya wanawake wakiwa wamejitokeza katika maadhimisho hayo. 

Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu "Wekeza kwa Mwanamke: kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa jamii" yamefanyika leo tarehe 08 Machi katika Viwanj a vya Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Wanawake waliojitokeza katika maadhimisho hayo, RC Malima, amesema siku hiyo ni muhimu kwa wanawake kwani  huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii.

Aidha, RC Malima, katika suala la  malezi ya watoto, amewataka wazazi/walezi  kuwalea watoto katika maadili mema ili kuwaepusha kujiingiza kwenye mambo maovu ya panya road na ushoga na ukatili wa kijinsia yanayoendelea kwenye jamii yetu.

"Nachukizwa sana na vitendo vya ukatili, katika mkoa wangu sitamvumilia yeyote atakayefanya vitendo hivyo, tunataka Mkoa wetu uwe safi na wale wanaofanya hivyo nitakula nao sahanai moja iwe mchana iwe usiku" Amesema RC Malima.

Kwa mkoa wa Morogoro , maadhimisho hayo yamefanyika  kimkoa Manispaa ya Morogoro  eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege  na kuhudhuriwa na Taasis mbalimbali zikiwemo  Taasis za Serikali na zisizo za Serikali.

Katika maadhimisho hayo mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na wanawake mkoa wa Morogoro yalibainishwa. na wanawake waliaaswa kuhakikisha wanapiga hatua zaidi katika kushika nafasi za uongozi. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebecca Nsemwa, amesema kuwa serikali inachukuwa jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote na kuondoa umaskini kwa wanawake na wasichana.

"Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote, pamoja na kuondoa umaskini kwa wanawake na wasichana na kuanzisha programu mbalimbali za kumuwezesha wasichana kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu ili kumuwezesha mtoto wa kike kuwa mwanamke shupavu na mwenye uwezo" Amesema DC Nsemwa.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.