Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAKUSANYA MAPATO ASILIMIA 100 MWAKA FEDHA 2022/2023


HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefanikiwa kufi kia lengo kwa kukusanya mapato ya ndani ya Sh bilioni 12 .653 ambayo ni sawa na asilimia 100 ya makisio yaliyowekwa ya Sh bilioni 12.654 mwaka wa fedha 2022 /2023.

Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amesema hayo katika Mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika Juni 30/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro.

Mhe. ametaja mikakati ambayo Manispaa iliweza kufanikisha ukusanyaji huo,ammbapo miongoni mwa mikakati hiyo ni utoaji elimu kwa walipakodi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na ushuru kwa ustawi wa maendeleo ya wananchi na kikosi kazi maalumu cha ufuatiliaji wa mapato ambacho kimeanza eneo la Msamvu.

Kihanga amesema  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, serikali kuu imetoa jumla ya Sh bilioni 8.497 ambazo ni saw ana asilimia 93 ya makisio ya Sh bilioni 9.115 ya mwaka wa fedha 2022/23.

Aidha, Mhe. Kihanga, amesema  miongoni mwa fedha hizo sh bilioni moja ni ujenzi wa Hospitali ya wilaya kwa kujengwa majengo manne ambayo ni wodi ya wazazi, mionzi, kufulia, jengo la dawa ambayo yapo yapo hatua za umaliziaji.

Kihanga amesema  sehemu nyingine ya Sh milioni 50 zimetumika ujenzi wa wodi ya wazazi kwenye Zahanati ya Konga ambapo jengo hilo lipo hatua ya umaliziaji.

Katika hatua nyingine amesema , Manispaa imetumia Sh milioni 555 ambazo ni sehemu ya mapato ya ndani kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kimoja na zahanati nne ndani ya manispaa hiyo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma ,                                       amewataka Madiwani pamoja na watumishi wa Manispaa ya Morogoro kuwa kitu                                   kimoja ili kuweza kufanikisha kwa ufanisi bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Charles Mkumbachepa ,amesema bajeti ya Manispaa ya mwaka wa fedha 2023/2024 inalenga kutatua changamoto za wananchi pamoja na kufanikisha ndoto ya Manispaa kuwa Jiji.                           

Dwani wa Kata Mindu, Zuber Mkalaboko amechangia  hoja mapato na kushauri  Menejimeti ya Manispaa kuandaa mikataba inayoziba mianya ya kuzalisha madeni dhidi ya wapangaji.

Pia kutumia mifumo ya kielektroniki ya tehama katika uendeshaji wa vitenga uchumi vya Manispaa ili kudhibiti masuala ya rushwa, upendeleo na uzalishaji wa madeni.

Diwani wa kata ya Mafisa, Joel Kisome amesema  bado Manispaa inapoteza mapato kwa sababu ya usimamizi usiofaa unaoweka vigezo wapangaji mpya kulipa madeni ya nyuma kabla ya kukabidhiwa vyumba vya biashara Kisome ametoa  mfano katika kituo cha mabasi cha Msamvu vyumba vingi vya biashara vimefungwa kwa kukosa wapangaji wapya licha uhitaji mkubwa kutokana na masharti yaliyowekwa jambo ambalo hawajibiki nalo.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.