MBUNGE MZERU AFURAHISHWA NA ASILIMIA 77 YA WANAWAKE KUAJIRIWA KIWANDA CHA NGUO MAZAVA MOROGORO
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Mzeru, ameoneshwa kufurahishwa na wingi wa ajira kwa wanawake katika Kiwanda cha nguo cha Mazava kilichopo Manispaa ya Morogoro.
Pongezi hizo amezitoa Juni 05/2023 katika ziara yake ya kutembelea Kiwanda hicho huku akisema , Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, imejikita sana katika Kujenga na kukuza uchumi shindani hususani kupitia sekta za viwanda na huduma za kiuchumi utakaowezesha ustawi wa wananchi wote.
Aidha ,Mhe. Mzeru, ametoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea watanzania maendeleo kwa kuhakikisha anatimiza malengo ya Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020-2025.
Mzeru, ametoa shukra za dhati kwa Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, na timu yake kwa namna wanavyopambana kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 ya Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango stahiki katika maendeleo ya nchi yetu.
" Ndugu zangu wana Mazava,nimekuja hapa kwa malengo mahususi kwani katika swali langu nililoliuliza Bungeni lililenga Kiwanda hiki kwa kutaka kujua ni lini Viwanda ambavyo wawekezaji wamewekeza hususani hapa Mazava watatengewa maeneo maalum ya akiba ya ardhi na uwekezaji ili watoke kwenye kulipa kodi ya pango wawe na maeneo yao kwani wamekuwa wakichangia sana ajira kwa Vijana wetu, changamoto nilizoziona nitazifikisha kwa Waziri husika na suala la miundombinu nalo naondoka nalo nitalipatia majibu" Amesema Mh. Mzeru.
" Nilichofurahishwa sana hapa mimi ni Mbunge wa wanawake , kiwanda kuajiri asilimia 77 ya wananwake katika waajiriwa 2600 kwangu ni faraja kubwa sana kwani wanawake wana dhamana ya kulea watoto tukiwasaidia hawa tumesaidia jamii nzima , kwahiyo ujio wangu ni kuoana namna ya kuwatetea wawekezaji kupatiwa maeneo ya uwekezaji, ambapo hapa Mazava mmekuwa mkizalisha ajira nyingi za Vijana , kama Mbunge wenu wa Morogoro nimeona hili niliseme Bungeni ili Serikali ione namna ya kuwasaidia wawekezaji" Ameongeza Mhe. Mzeru.
Hata hivyo, amewaomba wawekezaji wa Mazava kuendelea Kuboresha masilahi na mazingira
ya kazi kwa wafanyakazi ,kwani asilimia kubwa ya Vijana wanaofanya kazi katika
Kiwanda hiko wanatoka katika maisha duni
yenye vipato vya chini maslahi yao yakiwa mazuri wataweza kusaidia familia zao
kwa ufanisi.
Mbali na maslahi ya wafanyakazi , amewataka wawekezaji kuhakikisha wanaendelea kuboresha usalama
mahala pa kazi kwani sheria ya kazi inatutaka hivyo kwa ajili ya
usalama wa wafanyakazi kuwa salama kazini.
Sanjari na hapo, kikubwa alichotoa msisitizo zaidi ni wawekezaji kuzingatia usafi
wa mazingira, kama Taifa limekuwa likikabiriwa na mabadiliko ya tabianchi, hivyo
kuna kila sababu ya Viwanda kusaidia kuweka mazingira safi na salama.
Mwisho, amekipongeza Kiwanda cha Mazava kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uzalishaji wa bidhaa zenye ubora , huku akiwaomba kuongeza ubora zaidi
na kuongeza zaidi masoko , kwani uzalishaji unapoongezeka na masoko yanatakiwa
yaongezeke ili wafanayakazi waendelee kufanya kazi kuliko kuwa na uzalishaji
mkubwa na hakuna masoko itapelekea tena Vijana kupunguzwa kukaa mtaani
bila kazi kutokana na kukosa masoko ya bidhaa.
Mwisho, Mchukya, aamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi anazofanya kupitia Viongozi aliowateua kwani serikali ya awamu ya Sita imekuwa ikidhamiria kwa dhati kuwatenegenezea mazingira rafiki wawekezaji.
Post a Comment