Header Ads

HALMASHAURI ZA MKOA MOROGORO ZA PONGEZWA UBORESHAJI HUDUMA ZA AFYA







HALMASHAURI za Mkoa wa Morogoro zimepongezwa  kwa uboreshaji wa huduma za afya katika vituo  vyao vya kazi.

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi  wa Afya idara ya Afya, ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dr. Irene Haule, Juni 08/2023 katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.

" Nikupongeze Mganga Mkuu wa Mkoa na timu yako ya wataalamu wa afya kwa kazi nzuri ya kuboresha huduma za afya, nimefanya ziara tumejionea mabbadiliko makubwa hususani katika utoaji wa huduma, ubora wa huduma na miundmbinu mnastaili pongezi sana , lakini suala la usafi katika vituo vyenu vya afya nalo lipewe kipaumbele ili kuzuia milipuko ya magonjwa  na kuweka usalama kwa wateja wetu " Dr. Haule.

Pia , nimpongeze Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Charles Mkumbachepa na timu yake ya wataalamu kwa kuboresha huduma ya afya lakini kwa kufunga mifumo ya ukusanyaji wa Mapato jambo ambalo Manispaa kwa upande wa afya imejipanga kukusanya mapato.

Aidha, Dr. Haule, amezitaka CHMT kushiriki katika hatua za ujenzi wa miradi ya afya ili na wao watoe utaalamu wao kwani yapo maeneo ambayo wao wanaweza kushauri kama wataalamu wa afya kuliko kusubiri miradi kumalizika na kulalamika.

Hata hivyo, pongezi kubwa amezipeleka Manispaa ya Morogoro kwa usimamizi mzuri wa miradi ya afya kwa kutumia mapato ya ndani  ambayo miradi hiyo imeonesha ubora wa miundombinu  pamoja na thamani ya fedha.

Mwisho, amewataka wataalamu katika ujenzi wa miundombinu ya afya, ni vyema wakazingatia ramani za Wizara pamoja na miongozo ya ujenzi kuliko kujijengea bila kufuata miongozo.

Naye, Mratibu wa Chanjo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseline Ishengoma, ameupongeza Mkoa wa Morogoro katika upande wa afya kwa kuboresha huduma za chanjo pamoja na kuwahi kuwasilsiaha taarifa za chanjo Wizarani tofauti na vipindi vya nyuma.

Kwa upande wa Mratibu wa huduma za radiolojia TAMISEMI, Michael Tuhoye, amezitaka Halmashauri kupitia idara za afya kuhakikisha wanakagua mara kwa amara dawa amabazo zimeshaisha muda wake na kufuata taratibu ya kuziteketeza.

Pia amewataka wataalamu wa afya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya na vifaa tiba, pamoja na kuzuia upotevu wa vifaa hivyo kwani watakaogundulika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mratibu wa Kitengo cha Watu wenye ulemavu ,Haroun Haroun,  amewataka watu wa Ustawi wa Jamii kuhakikisha changamoto za wazee zinafanyiwa kazi katika kuboresha ustawi wa wazee pamoja na kuzingatia suala la lishe kwa jamii ili kuepukana na jamii yenye udumavu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dr. Urio Kusirye, amepongeza ziara ya TAMISEMI kwani ziara yao itazaa matunda makubwa na kufanya uboreshaji mkubwa wa Sekta ya afya kwa Mkoa wa Morogoro.

Dr. Kusirye, ameiomba TAMISEMI kuangalia sana changamoto ya Maji, umeme pamoja na majokofu ya kuhifadhia vifaa vya chanjo kwani changamoto hizo zinadumaza huduma za afya.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.