MANISPAA YANG'ARA MASHINDANO YA UMISETA MKOA WA MOROGORO 2023
MASHINDANO ya UMISETA kwa shule za sekondari Mkoa wa Morogoro ya kutafuta timu zitakazo unda timu ya Mkoa wa Morogoro yamemalizika kwa timu za Manispaa zilisoshiriki katika mashindano hayo kufanya vizuri katika michezo mbalimbali.
Fainali za mashindano hayo ya kusaka timu za Mkoa zimefanyika katika Viwanja vya Mpira wa Miguu Shule ya Sekondari Morogoro Juni 10/2023.
Akizungumza mara baada ya michezo hiyo kukamilika, Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Asteria Mwang'ombe, amesema Mnispaa ya Morogoro ilishiriki katika michezo ya Mpira wa Miguu wasichana na wavulana , Volleyball, Netball , pamoja na mchezo wa Handball.
Mwang'ombe ametaja matokeo ambayo timu za Manispaa zilipata katika mashindano hayo ambapo katika upande michezo ya Juni 08/2023 mchezo wa Volleyball Wavulana mechi ya kwanza Manispaa ilishinda seti 2 -0 dhidi ya Mlimba, Mpira wa Miguu mechi ya kwanza Manispaa ilishinda 6-1 dhidi ya Malinyi, Netball Manispaa 28- 10 Malinyi, Volleyball wavulana mechi ya pili Manispaa seti 2- 0 Moro DC , Volleyball wavulana mechi ya tatu Manispaa seti 2-0 Kilosa, Handball Wavulana Manispaa 0-4 Gairo, Mpira wa Miguu mechi ya pili Manispaa 4-1 Kilosa, Handball wavulana mechi ya pili Manispaa 5-19 Mvomero ,Mpira wa Miguu wasichana Manispaa 0-0 Malinyi na Mpira wa Miguu wasichana mechi ya pili Manispaa 1-1 Kilosa.
Katika michezo iliyochezwa Juni 09/2023, Volleyball wasichana Manispaa 2-Ifakara 0, matokeo ya Netball hatua ya makundi Manispaa 28-10 Ulanga, Manispaa 21-5 Gairo, Manispaa 23-8 Mlimba, makundi ya Basketball wasichana Manispaa 10-Moro DC 14, Mpira wa miguu Manispaa 1-1 Mlimba , Manispaa 0-0 Mvomero na upande wa Mpira wa miguu wasichana Manispaa 1-1 Mvomero.
Akifafanua zaidi kwa washindi wa michuano hiyo, upande wa Volleyball wasichana wamekuwa washindi wa kwanza (1), Volleyball wavulana washindi wa kwanza (1), Netball washindi wa kwanza, Basketball wavulana washindi wa pili (2) na Basketball wasichana washindi wa pili (2).
Katika upande wa michezo mpira wa Miguu, Mwang'ombe amesema Manispaa ilitakiwa kucheza kuwania nafasi ya mashindi wa tatu lakini mchezo huo haukuweza kufanyika.
Post a Comment