MBUNGE ISHENGOMA ACHANGIA MILIONI 5 UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI ,
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Christine Ishengoma, amechangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini inayotarajiwa kujengwa eneo la Kata ya Lukobe.
Kauli ya kuchangia ujenzi huo, imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Victoria Saduka, katika Baraza la kawaida la UWT lililofanyika Ukumbi wa CCM Kata ya Mji Mkuu Juni 10/2023.
Akizungumza na wajumbe wa Baraza, Saduka, amesema licha ya Mhe. Ishengoma kutofika katika Baraza hilo kama mgeni rasmi lakini amechangia kiasi cha Sh Milioni tano (5) ili kuwashika mkono katika hatua hiyo ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT.
Saduka,amesema,Jumuiya ya UWT imekuwa haina nyumba ya mtumishi hivyo kukamilika kwa nyumba hiyo utaepusha usumbufu wanaoupata makatibu wa Jumuiya hiyo pamoja na gharama za maisha.
Hata hivyo, Saduka, katika kuunga mkono Juhudi za Mbunge Ishengoma ,na yeye ameahidi wiki Ijayo ya mwezi Juni , 2023 atapeleka mchanga lori 5 pamoja na wajumbe 3 wa kamati ya Utekelezaji ambao wamehaidi Milioni 1 na mjumbe mmoja kuahidi shilingi 300,000/=.
Katika kuimarisha uhai wa Jumuiya, Saduka, amewataka Viongozi kufanya vikao vya kikanuni na vya kawaida, kuanzisha miradi pamoja na uwajibikaji wa watendaji kwani uchaguzi umeisha hataki maneno na malumbano badala yake viongozi waliochaguliwa wafanye kazi za Chama.
" Ipo Minong'ono kwa Viongozi , sitaki hizo kelele fanyeni kazi mlizoomba, na pia wapo viongozi tuliowachagua tuwaache wafanye kazi muda wa uchaguzi bado ,muda ukifika mtawapima kwa utendaji wao kwa sasa waacheni wawatumikie wananchi kama unamgombea wako subiria uchaguzi, Chama kina tarartibu zake " Ameongeza Saduka.
Aidha, Saduka, amewataka Makatibu wa Kata kutoingiza Mamluki katika Jumuiya hiyo kwani kukubali kuingiza mamluki watakipelekea chama na Jumuiya kugawanyika na kutengeneza makundi ambayo yatakuja kukigharimu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025.
" Tumefanya uchaguzi wa maeneo ambayo hayakuwa na Viongozi na tumepata viongozi wapya lakini nitoe rai kuwa Wapo baadhi ya viongozi wamekuwa na tabia ya kupanga safu za uongozi ambapo wamekuwa wakiwanyima wanachama wengine fomu makusudi nitumie nafasi hii kuwaonya viongozi wenye tabia hiyo kila mwana jumuiya wa UWT ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa"Amesema Saduka.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Twalib Bellege, kaitoa salamu za Chama, amezitaka Jumuiya zote za Wilaya kujiimarisha kiuchumi, kuimarisha uhai wa Jumuiya, pamoja na kuongeza kasi katika zoezi la usajili wa wanachama kwa njia ya kielektroniki.
Bellege, amesema , CCM Wilaya ya Morogoro Mjini ina jumla ya wanachama elfu 66 , kati ya wanachama elfu 34 wamesajiliwa katikia mfumo na wanachama elfu 32 hawajasiliwa.
"Tayari tupo na mpango kabambe ambao tutatumia miezi 2 kukamilisha zoezi la usajili, tumejipanga tuna simu 23 ambazo tutazitumia kwanza tutaanza kushuka hadi kwenye Matawi timu nzima pamoja na mashina yake baaada ya hapo tutakuwa tukiendelea Kata kwa Kata kwa kutumia mgawanyo huo wa majukumu , kazi iliyopo mbeleni kwetu ni kuhamashiha wananchama wajisajili ili waingie katika mfumo " Amesema Bellege.
Kwa upande wa Katibu wa UWT Mkoa wa Morogoro, Mwajabu Maguluko, amelipongeza Baraza hilo huku akiwataka Viongozi wa Jumuiya waongeze nguvu katika usajili wa wanachama.
"Morogoro wanachama wengi wanaonekana wapo hai kwenye reja lakini tukija katika mfumo bado tupo nyuma, viongozi tusilale twendeni tukaifanye hii kazi kwa spidi kubwa sana ili wanachama wetu waweze kusomeka katika mfumo" Amesema Maguluko. ,
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi, Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Bi. Judith Usaki, amesema katika ujenzi huo Madiwani wa iti Maalum kila mmoja atachangia 1250000 , Kamati ya utekelezaji kila mmoja 100000 na kuangalia namna gani wataweza pia kuwashirikisha Viongozi wa Kata katika michango hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu.
"Wakati tukiendelea na zoezi la ujenzi wa Nyumba ya Katibu, tunaendelea na kuimarisha uhai wa Jumuiya kwa kugawa kadi kwa wananchama wapya , kusimamia utendaji kazi wa Viongozi pamoja na kusimamia miradi ngazi ya Kata lakini kuhimiza zaidi kila Kata kufungua akaunti za Benki kupitia vikao vyao vyenye mihutasari ya kufungua akaunti hizo zikiwa na saii za wajumbe wao wa Kamati ya utekelezaji, hatutaki kushika hela mbichi, fedha zote zipitie benki huu ndio utaratibu ambao Chama kimetuelekeza" Amesema Usaki.
Usaki, ametoa pongezi kwa Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro , Mhe. Ishengoma, Mbunge Norah Mzeru, Sheilla Lukuba, Jane Mihanji , Haliya pamoja na wajumbe wa Kamati ya utekelezaji, Madiwani wa Viti Maluum Manispaa ya Morogoro bila kumsahau Mwenyekiti wake Victoria Sdauka kwa michango yao ya kufanikisha Baraza lao.
Aidha, Usaki ,amechukua nafasi ya kuwapongeza Madiwani wa Viti Maalum Manispaa ya Morogoro kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwatumikia wananchi pamoja na kujitoa katika Jumuiya hiyo hususani akimpongeza sana Mhe. Mwanaidi Ngurungu kwa ahadi za kadi 1000 kwa ajili ya kuimarisha uhai wa Jumuiya.
Post a Comment