VIONGOZI UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI WAPIGWA MSASA.
VIONGOZI WA UWT Wilaya ya Morogoro wametakiwa kuzingatia itifaki na uwajibikaji katika Kutekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo imetolewa na Viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Morogoro pamoja na Viongozi wa Chama Wilaya katika semina elekezi ya kuwajengea uwezo makatibu , pamoja na Wenyeviti wa Kata zote 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Viongozi waliohudhuria Semina hiyo, Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Morogoro , Ndg. Abiudi Shila, amesema lengo kuu la semina hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi hao katika kutimiza majukumu yao ya kiutendaji.
Shila, amesema suala la miradi ni muhimu sana pamoja na viongozi kuwa na vitabu ambavyo vitaonesha dira ya kujua mapato na matumizi na kutaka fedha zote zipitie Benki na sio kuwekwa mikononi mwa watu.
Kuhusu suala la ada za wanachama , Katibu wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Ndg. Zuberi Mtelela, ametawataka viongozi kuliwekea mkazo suala hilo huku akisema wale walioficha kadi kwa ajili ya kujipanga na kura za maoni basi wataumbuka na kadi zao hazitafanya kazi bila kuingia katika mfumo wa usajili wa kielektroniki.
Mtelala, pia amewataka Viongozi wanapofanya mabaraza basi mabaraza hayo yawe yenye tija kwa Jumuiya na sio mabaraza yenye lengo la kutaka kuwanufaisha watu wachache ( mabaraza ya mchongo).
Aidha, amewataka Viongozi kupendana na kujengeana mahusiano mazuri baina ya Viongozi wa Chama na wa Serikali ili miradi na changamaoto za wananchi ziweze kutatuliwa kwa wepesi.
Katibu UWT Mkoa wa Morogoro, Mwajabu Maguluko, amewataka Viongozi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, miiko pamoja na misingi ya chama hicho sambamba na kufanya kazi kwa mashirikiano ili kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya CCM.
" Niombe sana viongozi epukeni kupikiana majungu na kufitiniana na badala yake fanyeni kazi kwa kushirikiana pamoja kwa kuwashirikisha vingozi wa serikali na Chama katika ngazi za Mikoa na Wilaya wakati wakitekeleza majukumu yao" Amesema Maguluko.
Katika hatua nyengine, Maguluko, amewataka Viongozi wa UWT , kuitisha vikao vya kisheria , vya dharura na vya kawaida ili kukijenga chama kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuandika mihutasari kwa kumkabidhi katibu wa ccm wilaya na taarifa hizo ziende kwa wakati na zenye ukweli.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Twalib Bellege, ambaye ni miongoni mwa wakufunzi waseminishaji, amesema Chama cha Mapinduzi kinaongozwa kwa kanuni hivyo semina ya leo itawasaidia viongozi hao kujua namna ya kufanya kazi zao ikiwemo kujua masuala ya itifaki katika chama.
Akizungumza na wajumbe , Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Victoria Saduka, amesema lengo la UWT kuwapiga msasa viongozi wake ni kuwafanya kuwa viongozi bora na wanaujuwa majukumu yao.
Saduka mesema kuwapa semina hiyo kwa viongozi pia inawafanya kujua majukumu yao lakini pia kunatoa fursa wana CCM kuwa kitu kimoja kwa kupendana na kujenga mshikamano.
Katika hatua nyengine, Saduka, amewataka wanawake hao kuachana na mikopo yenye kuwakandamiza (kausha damu ) badala yake wajikite na mikopo ya taasisi za fedha kwa kuunda vikundi vitakavyoweza kukopeshwa fedha.
Katibu UWT Wilaya ya Morogoro Mjini,Judith Usaki, amezitaka Kamati za utekelaji kuhamasisha wanachama wao kulipa ada na kujisajili katika mfumo huku akisema kadi zipo nyingi zinakuja.
kwa upande wao Viongozi walioshiriki katika semina hiyo, wamepongeza hatua hiyo ya kupewa semina maana zipo changamoto zilizokuwa zinawakabili kama upande wa itifaki.
Post a Comment