Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAPOKEA SHILINGI MILIONI 620,014,716 FEDHA ZA RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU.

 

HALMASHAURI  ya Manispaa ya Morogoro imepokea Ruzuku kutoka serikali kuu jumla ya shilingi  620,014,716.00 kwa mwezi April 2023.

Akizungumza Juu ya mapokezi  hayo ya fedha hizo za Ruzuku, Mkurugenzi wa  Manispaa ya Morogoro Ally Machela, ameishukuru Serikali kwa kuipatia Manispaa fedha za Ruzuku na kuahidi kuzitumia  kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Machela amefafanua mchanganuo wa fedha hizo kama ifuatavyo ambapo Tsh.40,736,000.00 kwa matumizi ya kawaida,Tsh 133,038,074.00 kwa matumizi ya Elimu bila malipo Sekondari, Tsh 86,901,203.00 kwa matumizi ya Elimu bila malipo ya Msingi,Tsh.119,770,000.00 kwa matumizi ya Mitihani ya kidato cha sita,Tsh.128,319,439.00 kwa matumizi ya Basket fund robo ya tatu,Tsh.81,250,000.00 kwa matumizi ya Ujenzi wa madarasa shule za msingi na Tsh,30,000,000.00 kwa matumizi ya Ujenzi wa uzio shule maalum.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.