MRADI WA "USIIPOTEZEE UCHAFU" UTALETA MATOKEO CHANYA YA USAFI- DKT LUSAKO
MKURUGENZI wa Taasisi ya Wezesha Mabadiliko (WEMA), Dkt. Lusako Mwakiluma, amesema mradi wa "USIUPOTEZEE UCHAFU" utaleta matokeo chanya katika nyanja ya usafi na Mazingira.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo uliofanyika Kata ya Uwanja wa Taifa, Dkt. Lusako, amesema mrad wameanzsiha mradi huo ili kutoa elimu na kuongeza uelewa juu ya madhara ya utupaji taka ovyo katika mazingira yanayotuzunguka.
Dkt. Lusako,amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kuhifadhi taka ngumu ili kupunguza madhara katika jamii, hivyo kupitia mradi huo yapo mabadiliko makubwa ya kimazingira yatatokea na kuufanya mji kuwa salama.
Aidha, amesema mradi huo uliambatana na ugawaji wa mapipa ya kuwekea taka mtaa kwa mtaa na pia madereva wa mabodaboda wamegawiwa vivazi(Reflector) ili kueendelea kuelimisha jamii ikumbuke ili isiupotezee uchafu.
"Tumeanzisha mradi huu chini ya WEMA, mradi huu ni endelevu wenye malengo ya kuweka mji safi , lakini katika kuona hizo taka zinapatiwa mahala kwa kuzintunza , tumegawa Mapipa ya kuhifadhia taka chini ya usimamizi wa kata ya Uwanja wa Taifa ambao ndio watakuwa na dhamana ya usimamizi wa mapipa hayo" Amesema Dkt. Lusako.
Katika zoezi hilo, WEMA waliweza kushirikiana na Viongozi wa Kata ya Uwanja wa Taifa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na mfanyakazi wao toka Ujerumani anayejitolea katika shirika hilo ajulikanye kwa jina la PIA.
Post a Comment