MWENGE WA UHURU 2023 WASISITIZA VIJANA KUCHANGAMKIA MKOPO WA ASILIMIA 10.
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023 Ndg. Abdallah Shaib Kaim amewataka vijana kujitokeza kuchukua mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri zote Hapa nchini kwa lengo la kuwainua vijana kiuchumi.
Ndg. Abdallah Shaib ametoa kauli hiyo Mei 13 mwaka huu alipotembelea kikundi cha Okoa vijana kilichopo kata ya Tungi katika Halmashauri hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na vijana hao.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa amesema Serikali inatoa fedhan yingi kupitia Halmashauri zake ili kuinua makundi maalum wakiwemo vijana, hivyo vijana wanatakiwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupatiwa mikopo hiyo na kiuchumi.
Aidha, ndg. Abdallah Shaib amebainisha kuwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali ni asilimia 4 kwa vijana, asilimia 4 wanawake na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu.
Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameipongeza Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu Mkoa Wa Morogoro kwa kutii agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango lililoelekeza Bodi za maji kupanda miti zaidi ya milioni 2 katika maeneo yao, ambapo leo Mei 13 wamepanda miti 2000 katika eneo la bwawa la Mindu Manispaa ya Morogoro.
Akitoa shukrani kwa Serikali awamu ya sita katibu wa kikundi cha Okoa Vijana Bw. Hallington Godbless amesema kikundi hicho kimepata mkopo wa Tsh. Milion 23,000,000 ambazo zimetumika kuongeza mtaji wa kuzalisha chaki, hivyo wanaishukuru serikali na kuwahamasisha vijana wengine kujiunga kwenye vikundi vingine ili wapatiwe mkopo.
Post a Comment