Header Ads

MTELELA AWATAHADHARISHA WAPIGA SHOTI JUMUIYA YA WAZAZI NA KUPIGA MARUFUKU MABARAZA YA MCHONGO.

 

KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Ndg. Zuberi Mtelela, amewataka wale wenye tabia ya kujihusisha na ugombanishi kwa Viongozi waache tabia hiyo mara moja huku akiahidi  kutowafumbia macho wenye dhamira ya kukwamisha Viongozi waliopo madarakani.

Hayo ameyasema Mei 20/2023 katika kikao kazi cha Viongozi wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Morogoro Mjini pamoja na Viongozi wa Kata wakiwemo Wenyeviti na Makatibu wa Kata wa Jumuiya Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya CCM Mji Mkuu.

Amesema wasumbufu katika Jumuiya watolewe na hata mvumilia mtu mwenye malengo ya kutaka kuidhoofisha Jumuiya ya Wazazi.

Hata hivyo, amewataka wanajumuiya kuheshimiana na kuheshimu mamlaka ya Viongozi na wale watakaobainika kufanya hivyo hawatakuwa salama huku akisema Mtelela wa sasa amekuja kivyengine.

Mtelela amesema,  wakati wa chaguzi zote huibuka makundi mbalimbali yenye dhamira na maslahi tofauti hivyo, amewataka wana Jumuiya ya Wazazi  CCM kurejesha umoja na mshikamano baada ya uchaguzi kukamilika.

“Kamati za utekelezaji  chukueni hatua kali za kinidhamu kuhakikisha nidhamu na mshikamano ndani ya Jumuiya yetu ya Wazazi  unarejea pindi inapotokea mgawanyiko na makundi,tuishi kwa amani na tusiingilie maisha binafsi ya watu , wanaopigisha shoti tunawajua na dawa yao ipo jikoni ndio maana leo wapo baadi yenu wameshindwa kufika walijua nitakachosema ”Amesema Mtelela.

 Akizungumzia suala la uhai wa chama,Mtelela, amewataka viongozi wenye dhamana kwa mujibu wa nafasi zao ndani yaJumuiya ya Wazazi  kutekeleza jukumu na kuongeza wanachama wapya ili kuendelea kukipa uhai chama hicho kiendelee kushika dola.

“Mtaji wa chama chetu ni kuongezeka wanachama wepya, kadi zipo  za kutosha leteni hela mchukue kadi na wale waliochukua kadi za CCM na kuzifisha niwaambie kadi hizo katika kura za maoni hazitatumika ,watakaoshiriki kura za maoni ni wale waliopo kwenye mfumo wa Elektroniki tu na si vinginevyo ” Ameongeza  Mtelela.


Vilevile, amewahimiza wana CCM kulipa michango kwa wakati badala ya kusubiri hadi vipindi vya uchaguzi vikaribie.


Katika hatua nyengine, amezitaka Jumuiya zote Mkoa wa Morogoro kuhakikisha zinaorodhesha miradi ya zamani iliyopatiwa hati, kuorodhesha miradi iliyosajiliwa na wapangaji na namba za malipo (Control number), kila Kata kuwa na akaunti benki, kila Wilaya, Kata na Matawi kuwa na miradi ya Jumuiya pamoja na kuorodhesha mashamba ya Jumuiya yaliyopo katika maeneo yao.


Pia amepiga marufuku mabaraza yasiyokuwa na malengo ya kujenga Jumuiya badala yake Jumuiya zijikite katika kubuni miradi na kuwa na vyanzo vya mapato. 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.