HALMASHAURI KUU CCM WILAYA CHAMWINO YAGOMEA TAARIFA UTEKEKEZAJI ILANI CCM KUTOKA KWA MKUU WA WILAYA
HALMASHAURI Kuu CCM wilaya ya Chamwino Tarehe 9-5-2023 ilifanya kikao cha kupokea Taarifa ya Utekelezaji Ilani ya CCM kwa kipindi cha Julai-Desemba 2022 makao makuu ya Wilaya Chamwino na kukataa kuipokea Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwenye Kikao na Katibu Tawala Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya baada ya Kubaini uwepo wa mapungufu mengi Ikiwemo udanganyifu wa Baadhi ya Taarifa kuhusiana na Miradi.
Akiongea na Mvumi TV, mmoja wa wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Wilaya ambaye hakupenda jina lake kutajwa amethibitisha wajumbe kuikataa taarifa hiyo na kutoa mfano katika Kata ya Makang’wa uliainishwa mradi wa ujenzi wa Nyumba ya mwalimu Taarifa inaonesha katika jedwali Fedha bado kuletwa na ukurasa wa mbele ndani ya Taarifa hiyo hiyo inaonesha ujenzi upo unaenda Sanjari na Ujenzi wa Nyumba ya walimu Shule ya sekondari Ikowa na umefikia 75% baada ya kufuatilia kwa kina ilibainika hata ujenzi wa nyumba ya Mwalimu Ikowa Sekondari ujenzi uko hatua ya Msingi ilihali kwenye taarifa inaonesha ni 75%.
Aliendelea kusema kuwa ipo miradi mingi sababu za kuchelewa kwake imetajwa ni Mvua lakini uhalisia ilipo miradi ni Barabara ya Lami hakuna kikwazo cha ubovu wa barabara wala Mvua ,
Kikao hicho cha Halmashauri kuu CCM Wilaya kilitanguliwa na Ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya kutembelea miradi 09 ndani ya majimbo yote mawili yanayounda Wilaya Chamwino Tarehe 3/4 - 5-2023 ambako nako inasemekana Haikufurahishwa na baadhi ya miradi ikiwemo *ucheleweshaji wake kukamilika.
Aidha, Mvumi TV imebaini kuwa katika ziara ya Kamati ya siasa kukagua miradi kamati ya Siasa haikufurahishwa pia na mradi wa Maji Mvumi Mission Wenye thamani ya zaidi ya Milioni 900 ambao kimsingi ulipaswa kuwa umekamilika Mwezi Novemba 2022 lakini hadi sasa bado katika Mradi huo ndipo ilipobainika kijumba cha kuweka Pampu ya kusukuma maji chenye mabati 10 tu kugharimu Milioni 12 kamati ya Siasa ilielekeza Takukuru na mkaguzi wa Ndani kujiridhisha juu ya gharama hizo.
Mvumi Tv ilifanikiwa kuzungumza na Mjumbe Kamati ya Siasa Wilaya Ndg Abdalah Omar , alikiri kuwa kuhusu mapungufu ya baadhi ya miradi na changamoto hizo kuonekana waziwazi ni dalili za kukwamisha wazi jitihada za Serikali awamu ya 6 katika kuwahudumia Wananchi na Kusisitiza kuwa Halmashauri Kuu CCM Wilaya imetoa Siku 14 kwa Mkuu wa wilaya na watendaji wa Serikali kurekebisha dosari hizo ndani ya muda huo na kuiwasilisha tena CCM kwa hatua za Vikao.
Alipopigiwa na Mvumi Tv katibu CCM Wilaya Chamwino , Chief Sylvester Yaredi, Kuhusiana na hali hiyo alikiri kuwepo kwa kikao Cha Halmashauri Kuu Wilaya lakini Aligoma kusema kilichojiri ndani ya kikao hicho na aliongeza kusema kuwa yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho yanabaki ndani ya vikao kwa utekelezaji Zaidi,
Post a Comment