WAFANYABIASHARA MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KULIPA LESENI KUEPUSHA USUMBUFU WA KUFUNGIWA BIASHARA ZAO.
MKURUGENZI wa
Halmashauri ya Manispaa Morogoro Ally Machela amewataka wafanyabiashara na kulipia
Leseni ya biashara, ili kuepuka usumbufu
unaoweza kujitokeza kwa kufungiwa biashara zao.
Ameyasema hayo Mei
23/2023 wakati akitoa maagizo kwa wataalam wa idara mbalimbalimbali kupita kwa
kila mfanyabiashara ili kukagua iwapo mfanyabiashara husika anakibali
kinachokubalika kisheria.
Aidha amesema iwapo
itagundulika mfanyabiashara yeyote ambaye amekiuka agizo hilo basi hatua
stahiki zitachukuliwa ambazo ni pamoja na kuamuru kufunga biashara kwa hiari
yake au kufungiwa na wataalam kwa muda hadi pale atakapokidhi vigezo vya
kuendele na biashara hiyo.
Kwa upande wa Afisa Mapato
wa Manispaa Morogoro Fatma Lwebangira, amewataka wafanyabiashara kutoa
ushirikiano kwa jopo hilo la wataalamu kwa kutoa maelezo sahihi juu ya
uendeshaji wa biashara zao ili kurahisisha zoezi kutumia muda mfupi na kuendelea na majukumu
yao ya kila siku.
Sanjari na kukagua vibali hivyo, jopo la wataalamu linaendelea kutoa elimu juu ya mfumo mpya wa tausi unaomsaida mfanyabiashara kusajili biashara yake kupitia mfumo huo ambao ni rahisi na wa muda mfupi ukilinganisha na utaratibu wa hapo awali.
Post a Comment